Home Kimataifa Shaffih Dauda kaichambua robo fainali Uruguay vs Ufaransa, utabiri wake je?

Shaffih Dauda kaichambua robo fainali Uruguay vs Ufaransa, utabiri wake je?

8711
0
SHARE

Baada ya mapumziko ya siku mbili tatu, mchakamchaka wa kombe la dunia unarejea kwa kishindo. Tunaingia hatua nyingine, ugumu wa mashindano unazidi na ushindani unaongezeka, hii ni robo fainali ya kombe la dunia 2018.

Wadau wa soka kila mtu na lake, yule anaipa nafasi timu hii huyu anaiamini timu nyingine kabisa yani kila mtu kivyake na sababu zake.

Shaffih Dauda yeye yupo kwenye chungu kabisa ambako msosi ndio unapikwa na kupakuliwa (Russia), anafatilia kila kitu kwa ukaribu kuanzia nje hadi ndani ya uwanja. Yeye pia ana mtazamo wake na sababu zake zinazoweza kufanana au kutofautiana na zako kuhusu mechi ya Uruguay dhidi ya Ufaransa.

Mechi ya kwanza ya kombe la dunia hatua ya robo fainali Uruguay dhidi ya Ufaransa ni mechi ambayo itatupa taswira kuhusu ushindani ambao tumeuona kuanzia hatua ya makundi na matokeo ambayo hayatabiriki.

Hakuna ambaye alitarajia bingwa mtetezi angeweza kuaga mashindano katika hatua ya makundi tena kwa kufungwa na South Korea, hakuna aliyeamini kwamba bingwa wa Ulaya Ureno ataaga mashindano mapema kwa kufungwa na Uruguay katika mchezo ambao Uruguay walikuwa on top.

Matokeo mengine ya kushangaza ni kuiona Sweden ilipofika, wengi walikuwa hawaipi nafasi kutokana na jina lake kuwa dogo. Kuna vitu vingi sana vya kujifunza. Kuwa na timu iliyojaa wachezaji wenye vipaji, majina makubwa haitoshi kupata matokeo.

Kitu cha tofauti ambacho nimekiona kwenye mashindano ya mwaka huu ni kujitoa na team work kwa baadhi ya timu na kupambana kupata matokeo kumezisaidia baadhi ya timu.

Uruguay ni miongoni mwa timu zilizoonesha discipline ya hali ya juu, ukuta wao mgumu kupitika ukiongozwa na Diego Godin na Jose Maria Gimenez hadi sasa timu yao imeruhusu goli moja pekee na wanakutana na Ufaransa ambayo imesharuhusu magoli manne.

Kikubwa ambacho Ufaransa walikionesha kwenye mechi yao dhidi ya Argentina ilikuwa ni kutokana na ubora wa Mbape, Pogba na Varane ambaye anaongoza safu ya ulinzi ni kwa sababu walikutana na Argentina ambayo ilikuwa ‘disorganised’ safu yao ya ulinzi ilikuwa na mapungufu mengi na kumpa mwanya Mbape kung’aa.

Sitegemei defence ya Uruguay kama itafanya makosa ya kizembe na kumpa mwanya Mbape kung’aa kama ilivyokuwa dhidi ya Argentina. Kwa hiyo itakuwa mechi ngumu ambayo ukiangalia Uruguay tangu mwanzo wanacheza kwa umakini mkubwa na kuhakikisha wanapata wanachostahili.

Wana-defend kwa block, wana-create kwa block na wana-attack kwa block kwa hiyo ukiangalia kuna block tatu wanapokuwa uwanjani. Hakuna mchezaji anayeonekana kumtegea mwenzake afanye jukumu fulani.

Ni kawaida kumuona Kavani anarudi nyuma kuja kuokoa, sio tu wakati wa mipira iliyokufa kwa sababu imezoeleka washambuliaji hurudi nyuma kusaidia eneo la ulinzi wakati timu zao zinapigiwa kona au mipira ya kutengwa inayokuwa karibu na goli. Hilo ni jambo la kawaida kwa Kavani na inaonesha spirit, unit na desire ya kupata matokeo katika mashindano haya.

Ni mechi ngumu ambayo ni ngumu kuitabiri, matokeo yanaweza kuwa ya kushangaza kwa sababu baada ya Ufaransa kupata matokeo dhidi ya Argentina watu wengi wamekuwa na imani juu ya Ufaransa na kusahau Uruguay ni timu ngumu ambayo 2010 ilifika nusu fainali, 2014 walifungwa na Colombia hatua ya 16 bora lakini mwaka huu wameshavuka 16 bona, ninavyoona mimi wanaweza kwenda hadi nusu fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here