Home Uncategorized RUS 2018: World Cup ya Mwaka huu haina Mabingwa

RUS 2018: World Cup ya Mwaka huu haina Mabingwa

8626
0
SHARE

Kuna kijana mmoja anaijiita Pacha wa bakayoko huko Instagram. Ni rafiki yangu wa siku za usoni tu. Hata hatuwaji kuonana. Aliandika waraka wake akasema.

Huenda hili hukuligundua lakini acha nikujuze basi ili nitimize wajibu wangu.

Nikamuuliza kaka kulikoni? Lipi hilo chakubanga mimi silijui?
Akaniambia njoo pembeni kaka nikusimulie hadithi chungu kwa mashabiki wa Messi na Ronaldo maana wakinisikia naongea kwa nguvu watasema nina gubu.

Nakumbuka Marehemu Mzee kiraia aliniambia ukivutwa shati usijikaze utaenda nyumbani na shati chakavu. Nikamfuata bwana Bakayoko.

Akaniambia
Hivi unajua kama Kombe la Dunia mwaka huu sio kwa ajili ya mabingwa?

Kidogo nikaguna!

Akasema “eeh ndo hivyo Kombe la Dunia halina mabingwa mpaka sasa”

Nikamwambia Bakayoko nina mambo mengi ya kufanya kaka naomba niende.

Akanivuta zaidi mkono akaniambia kwa sauti ya chini.

“Bingwa mtetezi wa michuano hiyo namaanisha si unataarifa kwamba katoka?”

Nikamwambia ndiyo Ujerumani najua hawapo amemaliza wa mwisho kwenye kundi lake.

Akanikumbusha tena

“Bingwa mtetezi wa michuano ya Ulaya (Euro) namaanisha Ureno nao si unajua wametupwa nje wakiishia hatua ya 16 bora?

Nikamwambia haswaa…..

Akanishika bega akaniambia

“Sio hao tu, bingwa mtetezi wa michuano ya CAF Cameroon unajua wanauza mbege tu.

Nikamwambia ndio lakini Senegal si alifikia hatua nzuri ya kuweza kufuzu wewe huoni kama Senegal wamefanya vizuri tu?

Taratibu kidogo nikaanza kumuelewa nikamwambia ndiyo na tulitegemea hao Senegal ndio wataondoa aibu ya timu za Afrika kufuzuu hatua ya 16 bora lakini wakapokea kichapo kwenye mchezo wa mwisho ndo ikawa kwaheri kwao.

Akanijibu kwa kebehi “Sasa kama Bingwa wako hajafuzu ulitegemea huyo Senegal angefika wapi?

Bado akawa anaendelea kukazia

“Bingwa wa michuano ya bara la Asia, Australia ambao walibeba taji hilo mwaka 2015 nao walimaliza kwenye nafasi ya mwisho kwenye kundi lake.

nikaanza kuguna. Akaniambia tena

“Kaka usigune, Mabingwa mara mbili mfululizo wa Copa America huko kwenye bara la Amerika ya Kusini, Chile si unajua hawakufanikiwa kabisa kufuzu kucheza michuano hiyo kwa mwaka huu?

Nikamwambia ni kweli hata Marekani bingwa wa Marekani ya Kaskazini nae alichamba wima.

kisha aliponichekesha aliponiambia

“Sasa unamtaka na bingwa wa Antaktika? huko hakuna mtu anayeishi”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here