Home World Cup RUS 2018: Takwimu zote za Kombe dunia hizi hapa!!

RUS 2018: Takwimu zote za Kombe dunia hizi hapa!!

7062
0
SHARE

60 Ni miaka imepita tokea kijana mdogo Pele kufunga mara mbili katika fainali hizi za kombe la dunia akiwa na na umri mdogo kabisa. Hatimaye rekodi hii imevunjwa na Kylian Mbappe.

48 Ni miaka imepita tokea timu kuruhusu kufungwa mabao mawili na kutoka nyuma kisha kuweza kushinda mchezo katika hatua ya mtoano. Belgium walitoka nyuma ya mabao mawili dhidi ya Japan na kushinda mchezo huo kwa 3-2. Mara ya mwisho West Germany, walitoka nyuma ya mabao mawili dhidi ya England na kushinda mabao 3-2 kule nchini Mexico 1970.

Magoli 31 kati ya 146 yaliyofungwa mwaka huu kule Russia 2018 yamefungwa kuanzia dakika ya 80.

28 idadi ya penati zilizopatikana mwaka huu. Huku zikifungwa 21 pekee.

Mechi 22 kati ya 56 zimeenda sare kipindi cha kwanza. Hata hivyo ni mchezo mmoja tu umeenda suluhu 0-0. ilichukua michezo 37 ili mchezo uende bila ya kufungana na hii ni rekodi mpya katika kombe la dunia.

17 michezo aliyocheza nahodha ya Mexico Rafa Marquez na kuvunja rekodi ya Diego Maradona. Amekuwa mchezaji wa kwanza wa Mexico kuvaa kitambaa cha unahodha katika makombe matano mfulululizo akishikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kufanya hivyo nyuma ya Antonio Carbajal and Lothar Matthaus.

10 hii ni idadi ya magoli mengi ya kujifunga na imevunja rekodi ya mabao 6 ya kule nchini France 1998. Mchezaji wa Morocco Aziz Bouhaddouz anashikilia rekodi ya kujifunga bao dakika ya mwisho zaidi katika kombe la dunia ikiwa ni dakika ya 95 dhidi ya Iran, huku Sergei Ignashevich, mwenye miaka 39 akiweka rekodi ya mchezaji mzee zaidi kujifunga.

7 hii ni michuano ambayo Mexico wametolewa katika hatua ya 16 bora huku wakiwa na rekodi mbovu ya kufungwa mabao 13 huku wakishindwa kupata bao lolote katika michezo yao yote dhidi ya Brazil.

6 Magoli yaliyofungwa na nahodha Harry Kane na kuifikia rekodi ya Maradona .

3 mechi 3, Mabao 3 kwa Yerry Mina na kuwa beki wa kwanza kuwahi kufanya hivyo.

0 hakuna mchezaji wa England anayevaa jezi namba 8 amewahi kufunga bao katika penati za mtoano katika historia ya kombe la dunia, Chris Waddle, David Batty, Frank Lampard na Jordan Henderson, 1990, 1998, 2006 na 2018

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here