Home World Cup RUS 2018: Ni Hazard au Neymar

RUS 2018: Ni Hazard au Neymar

8935
0
SHARE

Leo jumamosi, kutakuwa na mechi ya pili ya robo fainali, ya kombe la dunia, kati ya Brazil na Belgium, itakayochezwa Kazan majira ya saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Tunakuletea taarifa za timu zote mbili, kuelekea kwenye mchezo wenyewe.

Brazil- Casemiro atakuwa nje, baada ya kupata kadi nyingi za njano. Kocha Tite amethibitisha kwamba, Fernandinho atachukua nafasi yake katika kikosi kitakachoanza. Marcelo ameonekana kupona sababu hakuwa vizuri, na alikosa baadhi ya mechi zilizopita. Leo anaweza kuchukua nafasi yake. Douglas Costa amepona pia majeraha yake, lakini ataanzia benchi.

Belgium- Wanasubiri hali ya Januzaj, ambaye alikosa mechi dhidi ya Japan. Ni mchezaji wao pekee mwenye majeruhi.

Tite: Kama inaonekana nimetulia, ni kwasababu wachezaji wameniweka kwenye nafasi hii, kwa kucheza vizuri. Tuna ujuzi na uwezo wa kukaa na mpira kwa muda mrefu, katika eneo la tatu na la mwisho wa uwanja. Neymar, Gabriel Jesus, labda na firmino ambaye sio sana kufanya hivyo, na Taison pamoja na Willian, watatupa uwezo huo. Wote wanaweza kwenda mtu kwa mtu. Shukrani kwa uwezo wao wa kukaa na mpira.

Roberto Martinez: Kocha huyu wa Belgium amesema, hakutakuwa na siri yoyote kwenye mechi. Tunapaswa kulinda tunavyoweza, pia kuwasukuma Brazil wakati tuna mpira. Ni rahisi, na timu hii iko tayari kwa hilo. Kama ukitaka kuangalia mechi unayotaka katika kombe la dunia, ni Brazil. katika kuzingatia, mchezo wa kuvutia, ubora wao, akili ya mataji. Kitu kimoja, cha kufikiria ambacho ni muhimu, ni Brazil na Robo fainali.

Je, unajua kwamba?

Hii itakuwa mechi ya tano, timu hizi zinakutana.

Mechi ya mwisho ya Brazil, kushinda dhidi ya timu pinzani kutoka bara la Ulaya, katika mtoano, ilikuwa fainali dhidi Ujerumani mwaka 2002.

Belgium hawajafungwa mechi 23 zilizopita.

Vikosi vya timu zote mbili vinavyoweza kuanza.

Brazil- Allison,Fagner, Thiago Silva, Miranda, Marcelo, Paulinho, Fernandinho, Coutinho, Willian, Neymar, Jesus

Belgium- Courtois, Alderweired, Kompany, Vertongen,Carrasco, Maunier, De bryune, Witsel, Martens, Hazard, Lukaku

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here