Home World Cup RUS 2018: Jezi ya Shaffih Dauda yazua gumzo, Brazil wakifuzu kwenda Brazil

RUS 2018: Jezi ya Shaffih Dauda yazua gumzo, Brazil wakifuzu kwenda Brazil

10790
0
SHARE

Leo kuna kibonzo kinasambaa mtandaoni kwamba eti mwamuzi anamuuliza Neymar kwamba naona leo unainuka mapema kulikoni!

Kuna kitu niliwaambia watu hapa. Nilisema Ubelgiji wana ufanisi mzuri sana katika kuhakikisha kwamba kila mchezaji anafanya kazi yake ipasavyo. Hakuna mchezaji mkubwa wala mchezaji mwenye mambo mengi. Nilijua tu kwamba Brazil watakiona cha mtema kumi.

Takwimu

Hii ni kwa mara ya kwanza Mchezaji wa Brazil anayevaa jezi namba 8 anafunga bao tokea mwaka 2006 katika michuano ya kombe la dunia.

Kelvin De bruyne ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mchezo huku akiwa mchezaji wa 100 kufunga bao katika fainali hizi za kombe la dunia.

Kwa mara ya kwanza Brazil kutoka nyuma ya angalau mabao mawili na kushinda mchezo. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1958 walipowafunga Sweden mabao 4-2.
Haijawahi kutokea timu iliyofungwa bao zaidi ya moja kipindi cha kwanza kufunga bao katika michuano ya kombe la dunia.

Kuna mdau kaniuliza inakuwaje VAR kama hazifanyi kazi? Mwingine akajibu VAR imeshaonekana iko poa lengo ilikuwa kupunguza baadhi ya timu. mimi nakauliza ikiwemo Brazil? akajibu ndiyo! Akasema Wazungu walihakikisha mataifa ya America yanatoka. Kwa sababu tokea mwaka 1958 Brazil walipotwaa ubingwa wa kombe la dunia kule ulaya (Sweden) Kwao ilikuwa fedheha kubwa kombe la dunia kuandaliwa katika bara la ulaya kisha timu kutoka America kutwaa ubingwa huu.

Katika timu zilizobakia katika nafasi ya nusu fainali ni timu mbili tu zilizowahi kutwaa Ubingwa huo Ufaransa 1998 na England 1966. Ubelgiji imeingia katika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia kwa mara ya pili (1988).

Hii ni kwa mara ya 5 Brazil wanatoka hatua ya 8 bora. Hii ni kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1994 mchezaji anayevaa jezi namba 9 kushindwa kufunga bao lolote katika michuano ya kombe la dunia. Zinho alishindwa kufanya hivyo na Gabriel Jesus pia amekwama.

Nilipiga stori mbili tatu na Shaffih Dauda kuhusu mchezo wa leo. Kabla hajanijibu akaniambia leo nimegeuka kuwa staa huko. Nikamuuliza kulikoni!! Akaniambia mashabiki wa Ubelgiji walikuwa wanang’ang’ania jezi yangu!(Video ipo Instagram) Kisha akaniambia Brazil walikuwa na kikosi kizuri na walicheza vyema. Shida ni kwamba upishi wao ulizidi. Walikuwa na nyama nyingi na walizirosti poa lakini wakazidisha chumvi. Hasa mpishi wao Mwalimu Tittie. Hakukuwa na sababu ya kuwaacha benchi Firmino na Costa ambao kila mechi walioingia kutokea benchi walifanya kweli.

Brazil ilipendwa sana hata wale akina dada wasiojua kombe la dunia ni nini wao pia walikuwa Brazil. Sijajua kwamba waliambiwa Brazil akibeba hilo kombe zile nywele za Brazilian hair zitashuka bei ama nini.

Kikubwa binafsi yangu siwezi kuilaumu sana Brazil labda tu kasoro kidogo za mbinu za mwalimu. Jesus alikuwa namba 10 bora wakati anatokea Palmeiras. Guardiola akalazimisha kweli kumweka namba 9. Lakini bado alipata msaada mkubwa wa Sergio Kun Aguero. Ilibidi Gabriel apate msaidizi kama Firmino ili awe huru. Mwisho wa siku michuano hii tumemwona kama anarukaruka tu.

Watu wanalaumu pengo la Casemiro. Sio kweli nakataa. Kilichowafunga Brazil sio uwezo sana wa Belgium ila tu nafasi kadhaa za bahati na wakazitumia vyema. Brazil walicheza vyema mno. Walicheza vizuri sana. Kumbukeni kwamba leo hii Courtois wabelgiji kwa sasa wanamuona kama Messi wao. Brazil bahati haikuwa yao. Ubelgiji walikwenda uwanjani kuzuia matokeo. Hakukuwa na hilo pengo la Casemiro. Labda walimkosa de lima tu.

Wapo wajujai watakwambia Kdb kaupiga mwingi sana. Huo ni ujuaji tu. Asilimia 70 ya mashambulizi ya Ubelgiji yaliishia kwenye miguu ya akina Miranda. Sikuo a Ubelgiji ikimtawala Fernandinho. Shida ilikuwa basi. Timu ikipaki basi unahitaji kiungo mkabaji? Wa nini?

Tukutane St Petersburg. Naitwa Privaldinho unaweza kunichek Instagram pia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here