Home Uncategorized RUS 2018: Hawa Ufaransa wapo siriazi na kazi!

RUS 2018: Hawa Ufaransa wapo siriazi na kazi!

9647
0
SHARE

Wabongo bhana! Kuna mshkaji kaniambia biashara ya utumwa ingeendelea huenda leo tungekuwa tunashangilia ushindi wa taifa letu la Ufaransa. Inaonekana biashara ya utumwa imefanya leo taifa la Ufarannsa washangilie. Varane anaonekana mweusi kabisa, hawa akina Kante, Labile n.k. Mimi huwa roho inaniumaga kutawaliwa na Waingereza. Wafaransa wangetutawala leo ungesikia Priva Pogshayo anapiga pasi murua kwa Tarimo n.k.

Hii ni kwa mara ya pili wanafika hatua ya nusu fainali tokea watwae ubingwa katika ardhi yao ya nyumbani mwaka 1998. Mchezo wa mwisho wa Uruguay, wamekula mkong’oto wa mabao 2-0, hapa Nizhny Novgorod, Russia.

Mchezo utakaofuata Ufaransa watacheza pale St. Petersburg.

Ni Raphael Varane na Antoine Griezmann ndio waliowarudisha Wauruguay kwao.

Huu ni mwaka wa magolikipa kucjonesha tu. Fernando Muslera leo amejaribu kudaka mpira kwa ustadi wa aina yake lakini mpira kumbe ulipigwa kwa aina yake pia.

Kabla ya hapo safu ya ulinzi ya Uruguay ilikuwa imeruhusu bao moja pekee.

Uruguay walifeli kupunguza kasi ya ushambuliaji ya Ufaransa. Safu ya Ushambuliaji nayo ilicheza kama wafiwa baada ya kukosekana kwa Edison Cavan.

Kukosekana kwa Edinson Cavan, iilikuwa pigo kwa Uruguay. Hata Suarez mwenyewe anafurahi akiwa na pacha wake Cavan, Kocha wa Uruguay Oscar Tabalez, namna alivyoenda kucheza na Ufaransa ni tofauti na alivyocheza na Ureno. Kwanza, dhidi ya Ureno Uruguay walikuwa wanazuia nafas na walikuwa wanacheza kitimu sana kwa sababu walikuwa wanajua wakianzisha mashambulizi ya kushtukiza, kuna wanaume wawili mbele tena wanaoshirikiana vyema sana.Nilipenda jinsi walivyocheza na Ureno ila leo Tabalez aliamua kushambulia tu kwasababu hakuamini kama ile 4-4-2 ya double striker isingefanya kazi kwasababu mtu muhimu kama Cavan alikuwa anakosekana. Hali ya kujiamin ya Uruguay ilikosekana katika idara zote na wamekuwa na mapungufu kwenye mipira ya set- pieces.

Shaffih Dauda aliyekuwa akiishuhudia mtanange huu alisema walinzi wa Ufaransa walifanikiwa kwa asilimia 90 kumtoa Luis Suarez mchezoni. Waruguay huenda wasimsahau kabisa Hugo Lloris baada ya kuchomoa mashuti kadhaa. Kichwa safi cha Martín Cáceres kiliokolewa kwa ustadi wa hali ya juu na Loris.

France walitangulia mnamo dakika 40 baada ya Griezmann kupiga mpira wa adhabu baada ya Rodrigo Bentancur, kumfanyia madhambi Corentin Tolisso. Mkwaju ule wa Griezmann ulienda moja kwa moja kwenye kichwa Varane ambaye alipiga kichwa mithili ya risasi iliyofyatuliwa.

Antonie Griezman, amekuwa mchezaji wa kwanza, kufunga goli, na kutoa passi ya goli katika hatua ya mtoano, kwenye kombe la dunia, tangu Patrick Vieira dhidi ya Spain, mwaka 2006.

Mchambuzi wangu Bwana Admila Patrick anasema

“Uruguay walikuwa wanacheza zaidi kwa kujilinda zaidi na wakijaribu kutumia mpira mirefu. Ukiangalia kabisa eneo la kiungo walifeli kwa sababu walikutana na viungo bora kabisa duniani mtu Kama pogba Toliso kante hili ilipelekea zaidi kushindwa kutengeneza nafasi. Kipindi cha pili waliamka lakini mbinu zao hazikusaidia Uruguay. Walitegemea mpira mirefu lakini je swali lilikuwa linakuja wana watu wa spidi? jibu hapana muda mwingi alikuwa nyuma me nafikiri hivyo tu bro? Safu yao ya ulinzi haikucheza vizuri Kama siku za nyuma kwa sababu presha ya mchezo ukiangalia ufarnsa eneo la ushambuliaji kuna mbappe, Griezmann, walijarbu kutengeneza chache na kuzitumia

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here