Home Kitaifa Kim kajiuzulu TFF

Kim kajiuzulu TFF

9771
0
SHARE

Mshauri wa ufundi wa TFF kwa timu za vijana Kim Poulsen amejiuzulu nafasi yake.

Kim amezungumza na The Citizen na kusema amejisikia vibaya kuchukua  uamuzi huo ambapo anawaacha vijana wenye vipaji wa U-16, Serengeti Boys ambao walishinda ubingwa wa CECAFA kwa vijana wa U-17 mwezi Aprili mwaka huu.

Kim amesema alikuwa anafurahia maendeleo ya vijana licha ya changamoto alizokuwa akikutana nazo ndani ya TFF.

“Nasikitika kutangaza hivyo kwa sababu nawaacha vijana waliozoea kuwa pamoja kwenye kila hali. Wakati mwingine unalazimika kufanya maamuzi ambayo kila mtu atauliza kwa nini umeamua kufanya hivyo. Nawatakia kila la heri wachezaji wangu na wadau wa soka”-Kim.

Kim hakuwa tayari kutaja sababu iliyopelekea kujiuzulu: “Nilichohitaji kukueleza ni kuhusu kujiuzulu kwangu, kama itahitajika kueleza kwa nini labda itakuwa baadaye lakini kwa sasa ni maamuzi yangu kuhusu kazi yangu.”

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao hakuwa tayari kuzungumzia juu ya kujiuzulu kwa Kim. “Tuna ofisa habari wetu ambaye anaweza kufafanua jambo hilo, wasiliana naye tafadhali”-Kidao.

Ofisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema hana taarifa kuhusu kujiuzulu kwa Kim.

Mwaka 2011 Kim aliajiriwa kama kocha wa timu ya taifa ya vijana kabla ya kupewa majukumu ya kuifundisha Taifa Stars 2012 akichukua nafasi ya m-denmark mwenzake Jan Poulsen.

Mwaka 2014 mkataba wake ulivunjwa na uongozi mpya wa TFF ulioingia madarakani chini ya Rais wa wakati huo Jamal Malinzi. Miaka miwili baadaye (2016) Kim aliitwa kwa mara nyingine kuendelea na majukumu ya kuwa mshauri wa ufundi wa timu za vijana.

Mwaka 2017 akiwa na Bakari Shime, Kim aliisaidia Serengeti Boys kufuzu kushiriki fainali za AFCON kwa vijana wa U-17 nchini Gabon.

Source: www.thecitizen.co.tz

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here