Home Uncategorized RUS 2018: Huku Torreira kule Pogba, pale Griezmann hapa Cavani

RUS 2018: Huku Torreira kule Pogba, pale Griezmann hapa Cavani

8979
0
SHARE

Kesho Ijumaa, kutakuwa na mechi ya kwanza ya robo fainali kati ya Uruguay na Ufaransa. Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Nizhny Novgorod, majira ya saa 11 kwa saa za Afrika mashariki.

Timu zote mbili zipo kwenye viwango vizuri, lakini Uruguay ambao ni mabingwa wa kombe la dunia, mwaka 1930 na 1950, wanaonekana wana rekodi nzuri, baada ya kushinda mechi zote kwenye hatua ya makundi, huku Ufaransa mabingwa mwaka 1998, wakishinda mechi mbili na kutoa sare mechi moja. Uruguay wameshinda mechi saba mfululizo, na Ufaransa wamepoteza moja katika mechi zao, 16 zilizopita.Timu zote mbili zilicheza vizuri katika mechi zao za mtoano katika kombe la dunia.

Mechi ya kesho inaweza kuamuliwa kwenye eneo la kiungo, ambapo timu zote zitakuwa na upinzani wa hali ya juu sana.

Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez anapendelea zaidi mfumo wa 4-4-2, kwa maana ya kuwatumia wachezaji wawili katika safu ya kushambulia, ambao watakuwa Luis Suarez na Edinson Cavani, kama akianza mechi. Mara nyingi Suarez na Cavani wanapenda kuwaondoa mchezoji mabeki wa kati wa timu pinzani na pia kuna wakati wanatanua uwanja ili kuruhusu Nandz na Vecino au Bentacur wapige pass kuanzisha mashambulizi ya kushitukiza.

Uruguay wao watategemea kukaa nyuma ili waruhusu nafasi na kuanzisha mashambulizi ya kushitukiza. Walinzi wawili wa pembeni wa Ufaransa, Pavard na Lucas Fernandez watataka kupandisha mashambulizi, hivyo kwa hali yoyote Uruguay, watakuwa wanatumia udhaifu huo. Pia watajitahid kumuondoa mchezoni Pogba ambaye mara nyingi ameonekana bora akipewa uhuru wa kushambulia kama alivyofanya dhidi ya Argentina, katika ushindi wa 4-3. Nahodha wa Uruguay Diego Godin na mwenzake Gimenez, watahakikisha wanamnyamanzisha kimya Kylian Mbappe ambaye spidi yake na nguvu ni hatari zaid, hivyo Godin atatumia uzoefu wake wote ili kumzuia Mbappe, ambaye ni mchezaji wa pili ghali zaidi duniani.

Uruguay pia watatakiwa kuwa makini, kwa wachezaji wengine wawili ambao ni Pogba na Griezman ambao huwa wanabadilishana kwenye kuanzisha mashambulizi. Kiungo mkabaji wa Uruguay, Torreira, atahakikisha anashirikiana vizuri na Vecino na Nandz, ili kuwafanya akina Griezman na Pogba wasiwepo mchezoni.

Uruguay wanasifika kwa kuwa na nidhamu ya ukabaji na kuwa kitu kimoja wakati wanazuia, kama walivyofanya dhidi ya Ureno. Mchezaji mwingine atakayeangaliwa ni beki wa kushoto wa Uruguay, Diego Laxalt, ambaye anatarajia kufanya kazi ya ulinzi kama alivyofanya dhidi ya Ureno.

Uruguay lazima wakubali kumchezesha mshambuliaji hatari, Edinson Cavan ambaye, alipata maumivu ya mguu kwenye mchezo dhidi ya Ureno, maana Uruguay bila Cavani hawaonekani hatari zaidi kwenye eneo la kushambulia. Watakubali wampe hata kipindi kimoja ilimradi awaachie maumivu Ufaransa.

Kwa upande wa Ufaransa, kocha Didier Deschamps, anapendelea zaidi mfumo wa 4-3-3, ila akikutana na mpinzani ambaye ni mgumu, anabadili mfumo, hata wakati mechi inaendelea.Mfumo wake unakuwa 4-2-3-1 ili kuwa na idadi ya wachezaji wengi kwenye eneo la kiungo na kuendelea kutawala kiungo. Tukumbuke hata mechi dhidi ya Argentina, Pogba na Ngolo Kante walikuwa wawili kwenye kiungo, na Blaise Matuidi alikuwa kama vile anatokea pembeni, ila wakati timu haina mpira, Matuidi alikuwa anarudi kwenye eneo la kiungo,kuongeza mchango wa ulinzi, na pia wakati Pogba anapandisha timu, Matuidi anarudi kusaidiana na Ngolo Kante.

Ufaransa watategemea kukaa na mpira na kuumiliki pia ili kuwachosha wachezaji wa Uruguay. Uruguay watataka kulazimisha akina Pogba na Griezman, wapige zile pass za pembeni tu zisizokuwa na madhara.

Wachezaji wa Ufaransa wengi wana kadi za njano. Matuidi ataukosa mchezo wa kesho, kutokana na kupata kadi nyingi za njano. Pogba na Tolliso pia wana kadi za njano, watapaswa kuwa makini mechi ya kesho.Wanaweza kukosa mchezo mwingne wa nusu fainali, kama watafuzu. Olivier Giroud ana kadi ya njano.

Kocha Didier Deschamps hataweza kupumzisha wachezaji wake wote wenye kadi, atakubali tu kufikiria zaidi mechi ya robo fainali, maana ya nusu fainali haijulikani kama atafuzu.

Wachezaji watakaotazamiwa kufanya vizuri kwenye mechi ya kesho ni Kyliani Mbappe na mlinzi wa kushoto Laxalt.

Tutarajie mechi nzuri yenye kutumia nguvu, akili na ubunifu wa hali ya juu sana. Hutakiwi kukosa.

By Admila Patrick

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here