Home Tetesi za Usajili Usajili Kitaifa Kocha mpya wa Simba kiboko! Mtapata tabu sana

Kocha mpya wa Simba kiboko! Mtapata tabu sana

14068
0
SHARE

Wakati wa michuano ya Sportpesa kulizuka sintofahamu kuhusu mkuu wa dawati la ufundi la Simba. Ilisemekana kuwa Piere ametupiwa virago vyake. Zikawa ni stori ambazo hazikuwa na kichwa wala mguu. Ghafla zikazuka tena habari za Masoud Djouma kuwa ameshapewa nauli ya kurudi kwao Burundi.

Wanachama wa Simba wameishuhudia timu yao ikiwa chini ya Masoud Djuma kwenye michuano ya Kagame Cup bila kocha mkuu huku Lechantre akiwa tayari katimka zake. Ni kweli hatimaye Mbelgiji kocha Patrick Aussems ametua nchini na tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia wekundu wa msimbazi.

Sasa ni wazi Pierre Lenchantre hawezi kurudi tena klabuni hapo licha ya kuwapa ubingwa uliokumbatiwa na wanajangwani kwa kipindi kirefu.

Majina Kamili Patrick Winand J. Aussems
Tarehe ya kuz 6 Februari 1965
Sehemu kuz Moelingen, Belgium
Urefu 1.90 m (6 ft 3 in)
Nafasi ya kuch Mlinzi

Ametumia Muda mwingi sana katika klabu ya Standard Liege akiwa kama mlinzi wa kati.

Alichezea Vilabu hivi hapa
1974–1981 RCS Visé
1981–1988 Standard de Liège
1988–1989 K.A.A. Gent
1989–1990 R.F.C. Seraing
1990–1993 ES Troyes AC

Amekuwa kocha wa muda mrefu katika ligi za Afrika kama Cameroon na Congo kabla ya kutimkia Nepal.

Orodha ya Vilabu alivyovifundisha

Patrick Aussems mara ya mwisho amejiunga klabu ya Marbela United maarufu kama MUFC mnamo January 14, 2017 baaa ya miaka 30 ya uzoefu wa soka la Europe, Asia, na Africa. Aussems amecheza ligi daraja la kwanza huko Belgium na France. Pia aliwahi kuitwa timu ya taifa ya Belgium . Aussems’ anamiliki leseni ya UEFA (UEFA Pro License)

Kocha mkuu timu ya taifa ya Nepal

Patrick Aussems aliisaidia Nepal mwaka 2016 kushinda South Asian Games kule India, pia alitwaa kombe la Banganbadhu Gold Cup kule Bangladesh. Aliweza kuisaidia Nepal, kupanda viwango vya FIFA kwa alama 11 kutoka #192 to #181.

Kocha mkuu wa Benin

Aussems aliisaidia Benin kufuzu mashindano ya mwaka CAN 2008 kule Ghana, pia alifanya hivyo mwaka 2010 kule Angola. Pia aliisidia timu ya vijana ya U19 & U16 kushiriki michuano ya African Cup CAF mwaka 2009. Aliweza kuisaidia Benin kwenye viwango vya FIFA kuruka nafasi 55 , kutoka #114 mwaka 2006, hadi nafasi ya #59 mwaka 2009. Huyu anatufaa taifa Star huyu.

Kocha wa Madaraja ya 1st & 2nd huko Europe, Africa na China

Patrick mwaka 2014/15 aliisaidia Al Hilal Omdurman ya Sudan kushinda ubingwa Sudan Super Cup mwaka huo huo alifika fainali African Champions League mwaka 2015. Kabla ya hapo msimu wake 2013/14 Aussems alikuwa kocha mkuu wa AC Leopards Dolisie ya Congo ambapo alifanikiwa kutwa ubingwa wa ligi na alifanikiwa kufika fainali ya African Cup.

Kuanzia mwaka 2010-2012, Patrick Aussems alikuwa kule China kwenye ligi daraja la kkwanzana klabu ya Shenzhen Ruby, kisha akaelekea Chengdu Blades 2012.

Kule nchini Ufaransa Aussems alishinda National Championship akiwa na timu ya daraja la pili iitwayo ETG FC mwaka 2009/10. Hapo awali kuanzia mwaka 1997-2002, alishinda mataji mawili akiwa na SS Capricorne, na Saint-Louisienne.

Takwimu zake kama Mchezaji

Akiwa kama mchezaji amecheza michezo 250 ndani ya Belgium na France ndani ya miaka 17. Aliichezea timu ya taifa ya U23. Aussems amecheza michezo 20 ya UEFA Cup. Pia aliwahi kutwaa Belgian Super Cup na ubingwa wa Belgium.

Kuna mtu kaniambia huyo kocha asije akajichanganya akaja na begi kubwa maana Simba sio wavumilivu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here