Home Kimataifa Kadi 6 Uingereza v Colombia, lakini inashika nafasi ya ngapi katika mechi...

Kadi 6 Uingereza v Colombia, lakini inashika nafasi ya ngapi katika mechi za kitemi Wc?

7935
0
SHARE

Usiku wa jana dunia ilishuhudia kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia Uingereza wakifudhu kwa hatua inayofuata kwa mikwaju ya penati, lakini mchezo wa jana unatajwa kama mchezo wa kitemi zaidi World Cuo 2018, lakini je ni mchezo wa ngapi wa kibabe zaidi katika historia ya kombe la dunia.

1. Italy vs Chile 1962, mwaka huu ndio mwaka ambao Chile waliandaa kombe la dunia, mwamuzi wa pambano hili alikuwa Ken Aston raia wa Uingereza na mchezo ukiwa dakika za mwanzo tu fujo kubwa iliibuka na ngumi kuanza uwanjani hali iliyomlazimu Aston kutoa kadi mbili nyekundu kwa Italia, inadaiwa kuna mchezaji wa Italia alivunjwa pua kwa kiwiko na Chile wakaibuka kidedea kwa mabao 2-0.

2. Hispania 1 vs Uholanzi 0 (2010), hii ni mechi ambayo vijana wengi wanaikumbuka haswa faulo ya De Jong kwa Xabi Alonso lakini haswa Howard Webb maamuzi yake akiwalima wachezji 14 kadi za njano huku Johnny Heitinga akipewa kadi nyekundu.

3. England 1 vs Argentina 0 (1966), inadaiwa katika mechi hii wachezajia wa Argentina walikuwa wakiwatemea mate Uingereza na kuwavuta masikio muamuzi akigeuka pembeni, hali hii ilimuudhi sana kocha wa Uingereza wakati huo Alf Ramsey na kuwaambia wachezaji wake wasibadilishane jezi na Argentina aliowaita wanyama.

4. Italy 2 vs Argentina 1 (1982), target kubwa kwa Waitaliano siku hii ilikuwa ni kumzuia Diego Maradona, katika kipindi cha kwanza tu Claudio Gentile mlinzi katili wa Italia alishampiga viatu 23 Maradona na dakika ya 42 muamuzi alishindwa kumvumilia na kumpa kadi nyekundu.

5. Germany vs Uholanzi 1990, Frank Rijkaard  anatajwa kama chanzo cha fujo katika mechi hii baada ya kumtemea mate Rudi Voller baada ya Rijkaard kupewa kadi ya njano, baadae tena kulitokeoa fujo kubwa uwanjani na wawili hawa walionekana chanzo na ndipo muamuzi aliamua kuwapa kadi nyekundu wote wawili.

6. Ureno 1 vs Uholanzi 0(2006). Mimi binafsi katika umri wangu sitakuja kusahau hii mechi, ndio mechi yangu ya kitemi zaidi niliwahi kuona. Muamuzi Valentin Ivanov alitembeza kadi 16 za njano na nyekundu 4(mbili mbili kwa kila upande), lakini Ureno wakafudhu kwenda robo fainali kuikabili Uingereza.

7. Scotland vs Uruguay 1986. Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alisema Uruguay hawana utu, kitu kikubwa kinalalamikiwa na Scotland ni tukio la wachezaji wa Uruguay kusimama juu ya miguu ya wachezaji wa Scotland na kuzuga kama wanawapa msaada kumbe wanataka kuwavunja, katika mechi hii kadi nyekundu ilikuwa moja tu kwa Jose Batista na Uruguay akafanikiwa kupata suluhu iliyowavusha.

8. Ureno vs Brazil 1966. Ilikuwa nchini Uingereza na mchezaji nyota wa dunia katika kipindi hicho Pele alikuwa anatoka katika majeruhi, lakini Wareno waliamua kumkazia yeye na Joao Pinto alipewa kazi ya kumzima Pele, aliumia sana kiasi cha kushindwa kutembea na hadi sasa Pele anaamini hiyo ilikuwa mechi chafu kuwahi kuona, Ureno alishinda 3-1.

9. Cameroon v Argentina 1990, Waargentina waliokuwa mabingwa watetezi walipata tabu haswa siku hii, Cameroon walitumia nguvu kubwa sana kuwazima na hadi mchezo unaisha walipiga rafu 30 huku 12 kati ya hizo zikiwa kwa Diego Maradona, Wacameroon wawili wakala umeme lakini Cameroon ikawa timu ya kwanza ya Waafrika Weusi kushinda mechi kombe la dunia.

10. Colombia v Uingereza 2018, Diego Maradona amesema kilichotokea katika mechi hii ni wizi katika soka na muamuzi Mark Geiger alipanga kuwaumiza Colombia, kadi 8 za njano zilitoka huku Colombia wakila kadi 6 na Uingereza wanafudhu robo fainali kwa mikwaju ya penati.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here