Home Tetesi za Usajili Chelsea yanasa watatu

Chelsea yanasa watatu

10082
0
SHARE

Nyota watatu wa kikosi cha vijana cha Chelsea wamekamilisha kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Chelsea.

Billy Gilmour ambaye wiki kadhaa zilizopita alikuwa akitimiza miaka 17 toka kuzaliwa kwake amesaini mkataba mpya wa kuitumikia Chelsea akiwa kama mchezaji wa kulipwa. Gilmour ambaye anatajwa kama moja ya nyota wenye vipaji aliutumia msimu uliomalizika kama mchezaji wa klabu ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 18, Chelsea U18s na kuisaidia timu hiyo kushinda mataji manne kati ya matano.

Nyota mwengine kutoka nchini Ufaransa, Nicolas Tite ambaye ni mlinda mlango wa klabu hiyo ya vijana akiwa na miaka 17 amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu ukiwa unamalizika mwaka 2021.

Tite amekuwa akitajwa kufukuziwa na klabu ya Rennes ya nchini Ufaransa amesainisha mkataba huo akiwa kama mchezaji wa kulipwa.

Nyota mwengine aliyesaini mkataba mpya ni Daishawn Redan ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Chelsea akicheza nafasi ya ushambuliaji akiwa ni raia wa Uholanzi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here