Home Kimataifa A – Z ya sakata la uhamisho wa Cr7, chanzo ni nini...

A – Z ya sakata la uhamisho wa Cr7, chanzo ni nini na nini kitatokea?

14470
0
SHARE

“Its happening” ni kweli its happening/ inaonekana inaenda kuwa kweli, baada ya kuanza kama mzaha au tetesi hatimaye inaonekana Juventus wako serious na uhamisgo wa Cristiano Ronaldo.

Ronaldo kweli anataka kuondoka Real Madrid?

Wakati Cr7 aliposhinda karibia kila kitu na klabu ya Manchester United aliondoka kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto mpya, akiwa Madrid amechukua kila kikombe cha ngazi ya vilabu na pesa amechuma, anataka nini tena na kama sio kumalizia soka lake katika mji wenye mvinyo mtamu kama Turin?


Amedharauliwa.

Thamani ya Neymar kwa sasa ni zaidi ya £200m aliyonunuliwa PSG, Kane anatajwa kuwa na thamani zaidi ya £250m kwa sasa, lakini mwezi January wakati Real Madrid wakiweka kiwango cha pesa ambacho Cr7 anaweza kuondoka Real Madrid ilikuwa £100m (nusu ya Neymar), hii ilikuwa dharau kwa nyota huyu bora wa dunia na anahisi Madrid hawampendi tena.

Inafahamika kwamba ndoto ya Ronaldo ilikuwa ni kustaafu akiwa na Madrid, Zinedine Zidane alipambana kuhakikisha Ronaldo anafurahia maisha ya ndani ya Madrid lakini inatajwa kwamba kiwango chake cha raundi ya kwanza La Liga kiliwashtua mabosi na hawakusita kushusha thamani yake.

Juve vipi watatoa mzigo?

Jarida maarufu la michezo la Tuttospot liliweka wazi kwamba Juventus wako tayari kumnunua Cristiano Ronaldo, lakini waandishi wa habari wengi Italia hawaamini kama Juve wanaweza kumpa £100m mchezaji mwenye miaka 32 na kumlipa £26m kila mwaka kwa miaka minne(hadi afikishe 37).


Jorge Mendes naye vipi?

Hizi ndizo nyakati ambazo wakala wa Cr7 Jorge Mendez anakuwa maarufu kuliko mchezaji, lakini mbona hatumsikii? Kama unadhani Mendes yuko kimya baasi unajidanganya, inasemekana Mendes mwenyewe ndiye alimpa huu mchongo moja ya wakurugenzi wa Juventus bwana Fabio Paratici.

Lakini upande wa pili kuna mashaka kuhusu Mendes, amekuwa ni mchezeshaji sana linapokuja suala la kutaka maslahi yeye pamoja na mteja wake, inawezekana hii ikawa kampeni yake kutaka Real Madrid waongeze pesa wanazompa Cr7.


Real Madrid wanasemaje?

Waswahili wanaamini “kimya nacho ni jibu”, Real Madrid wako kimya. Pamoja na kutolea ufafanuzi wa tetesi nyingine kama suala la Neymar kwenda Madrid na Mbappe kwenda Real Madrid lakini kuhusu Cristiano Ronaldo wamekaa kimya na hakuna taarifa yoyote kutoka kwao.

Ni muuaji wa Juventus, mashabiki watampokeaje?

Kama hufahamu tu ni kwamba pamoja na kuwafunga bao matata la “overhead kick” msimu uliopita lakini badala ya mashabiki wa Juventus kusikitika, walimpigia makofi. Ronaldo aliweka mkono moyoni akiwashukuru na kukiri kwamba ni jambo zuri sana kwake na halijawahi kumtokea wapinzani kumshangilia. Tayari hii imejenga upendo kati ya mashabiko wa Juventus na Cristiano Ronaldo.


Magazeti nayo yanasemaje? 

“Ronaldo Ora Mai Piu” gazeti la Corriere limeamka na kichwa cha habari hicho na kwa tafsiri wanasema “Ronaldo its now or never” wakimaanisha huu ndio muda wa Juve kumnunua au wasahau.

“Operazione Cr7, Juve Boom” hao ni Tutto Sport na katika habari yao hiyo, ndani kuna sehemu inaeleza kwamba Jorge Mendes anataka kufanya mazungumzo na Florentino Perez kumaliza jambo hilo.

Marca nao hawako nyuma kwani katika makala ya muandishi Fillippo Ricci amesisitiza kwamba £100m ndizo ambazo zimemfanya Cristiano Ronaldo kujihisi hathaminiwi tena Real Madrid na anataka kuondoka.

Wewe una maoni gani kuhusu sakata hili?

Ni mda wa Ronaldo kuondoka au bado bado akipige Real Madrid?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here