Home World Cup RUS 2018: Honda, Hasebe Watundika Daluga Kuichezea Japan

RUS 2018: Honda, Hasebe Watundika Daluga Kuichezea Japan

7516
0
SHARE

KEISUKE Honda na Makoto Hasebe wametangaza kustaafu soka la kimataifa, mara baada tu ya kuondolewa katika fainali hizi za Kombe la Dunia mwaka 2018 zinazo endelea nchini Urusi.

Wachezaji hao wa timu ya taifa ya Japan wametoa tamko hilo, baada ya timu yao kupoteza mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ubelgiji. Kwa kupoteza kwa mabao 3-2 na kuifanya timu hiyo ya Samurai wa bluu kuondoshwa katika fainali hizo.

Katika fainali hizi za Kombe la Dunia mchezaji Honda, hakuwa chaguo la kwanza kwa kocha, ambapo alikuwa akimtumia kama mbadala wa pili akitokea benchi.

“Mchezo wetu dhidi ya Ubelgiji tulionyesha jinsi tunaweza kuendelea kama soka la Kijapani,” alisema Honda mwenye umri wa miaka 32, ambaye ameifungia mabao 37 Japan.

“Ninafurahi, kwa sababu tuna wachezaji wengi wazuri, na sasa ni wakati wao wa kuandika historia ya soka la Kijapani.

Pia nahodha wa Japan Hasebe ambaye pia ni mchezaji wa klabu ya Eintracht Frankfurt, alisema kwamba tayari amefikia mwisho wa kuitumikia Japana. Nahodha huyo ameitumikia Japan michezo 114.

“Ningependa kutoa shukrani kwa wenzangu ambao walipigana pamoja kwa muda wa miaka 12 na nusu tangu 2006, na kwa watu wote wa Kijapani ambao walisaidia sana.

“Lakini mwisho pia sitakuwa mbali na na timu hii, maana bado nitakuwa msaidizi wa timu ya taifa,” alisema Hasebe

~ *Official_DSK*

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here