Home Makala Arsenal wamefaulu somo la nidhamu, vipi kuhusu hesabu?

Arsenal wamefaulu somo la nidhamu, vipi kuhusu hesabu?

8955
0
SHARE

Kuna yule jamaa wa BVB mwenye jina gumu na refu kama mtihani wa hesabu anaitwa Sokratis nmepata taarifa kuwa sasa yule rasmi ni mchezaji wa Arsenal. Wazee wa kubeba ubingwa kabla ligi haijaanza. Wana pacha wao anatokea vijijini huko ambao wao wanakwambia ndo magwiji wa soka England nzima, Wanasajili kwa mbwembwe hao. Nimejiuliza sana kuhusu ufanisi wa Sokratis na uhitaji wa Arsenal.

Nmefuatilia kwa kina sana andiko la Ronan Murphy. Murphy ameonekana kusimamia pande mbili katika usajili huu. Upande wa kwanza Ronan anasema

“Mgiriki huyu ataleta chachu kubwa ya ushindani na ni alama sahihi ya nidhamu katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa Arsenal”

Naweza kukubaliana na Ronan kwa asilimia 10000. Nikiangalia kikosi cha Arsenal hakuna mhenga mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia nidhamu ipasavyo. Unakumbuka ule mchezo wa Man City dhidi ya Arsenal kwenye kombe la Carabao? Watu wengi walilaumu wachezaji wa Arsenal kwa kukosa nidhamu.

Marafiki zangu wa karibu wanaoshabikia Arsenal wana imani kubwa kwamba ule utoto utoto kwa sasa utaisha Arsenal. Pembeni watakuwa na Litchestner huku katikati akisimama Sokratis ambao wote ni wahenga. Sina uhakika sana na mawazo wa Unai kuhusu Belerin. Binafsi Belerin ana umuhimu mkubwa sana kwemye timu kwa manufaa ya kesho ila Liec ni wa muda tu.

Wadau wengi wa soka wanasema wanahitaji majina makubwa Emirates Stadium ili wasaidie kuweka motisha kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo.

Kila chumba cha kubadilishia nguo kinahitaji mtu kama Flamini, Rooney watu kama Puyol. Wachezaji ambao kutokana na muonekano wao au uwezo wao wa kuongea huwapa wenzake nguvu ya kupambana.

Bila shaka Sokratis ni chaguo sahihi. Sokratis alikuwa baba wa taifa pale Iduna Park. Hata alipokosea Aubameyang Sokratis alimtetea mbele waandishi wa habari. Auabameyang alipoondoka mashabiki wengi walimtukana sana lakini Sokratis alivaa viatu vya Aubameyang na kumtetetea.

Katika historia ya Wenger ndani ya miaka 22 kikosi chake bora kilijengwa chini ya watu kama hawa. Akina Tony Adams, Akina Lyumerg na Vieira. Watu ambao wanajua thamani ya medali ni nini. Watu ambao wapo tayari katika wakati ufao na wakati usiofaa.

Kocha wa zamani wa PSG Unai Emery ameanza na Sokratis Papastathopoulos ambaye bila shaka huyu amebeba picha halisi ya kiongozi uwanjani. Arsenal imejaa na wachezaji wazuri sana lakini nidhamu ya na hari yao ya upambanaji inashuka muda wowote. Yupo Shaka kichwa chake kipo mbele dakika 10, yupo Mkhitaryan ambaye ni mwepesi kususa. Hawa wote walimhitaji Sokratis asimame nyuma yao.

Je Unai atamkabidhi Sokratas unahodha ama lah! Ronan anasema kuna uwezekano huo kwani Sokratis amekuwa nahodha katika historia ya maisha yake ya soka. Alianiza AEK Athens alipokuwa nahodha mwemye umri mdogo katika historia ya klabu hiyo akiwa na miaka 19 tu. t

Amepata bahati ya kuvaa kitambaa cha unahodha kwa makocha wote wawili Peter Bosz na Peter Stoger msimu wa 2017-18 pale Borussia Dortmund.

Inawezekana kweli akawa nahodha. Anazo sifa zote. Wakayi Aubameyang aliposusia mazoezi ili aende Arsenal Sokratis alisimama na kusema

“Nakubaliana na sheria za timu. Ni kweli amekosea lakini tusisahau makubwa aliyofanya Aubameyang. Kila mtu anakosea. na hili ni jukumu la kila mmoja kumsaidia kwa njia yoyote atakayohitaji. Iwe ana hama au anabaki. Maisha ya mchezaji yapo hivyo. Hatupaswi kumchukia hata kama ataondoka. Maana hata sisi tuliopo hapa kuna mahali tuliondoka.

Sokratis ataungana na nahodha wa Uswisi Stephan Lichtsteiner

Arsenal imekuwa timu inayokumbwa sana na wimbi la wachezaji wengi kuhama. Aubameyang, alipokosa mazoezini akitaka kuondoka Msaidizi Bosz bwana Hendrie Kruzen alimjia juu Aubameyang na kudai kuwa mchezaji huyo ndio chanzo cha BVB kufanya vibaya.

Sokratis alisema “Siona kama kuna ulazima wa Auab kujibu. Mimi nimecheza BVB kwa miaka minne na kucheza michezo zaido ya 180 nilijitoa kwa moyo wangu wote. Auaba hapaswi kujibu hili nje ha uwanjan bali anapaswa kutekeleza wajibu wake ndani ya uwanja.

Upande wa pili ni kuhusu ufanisi wa Sokratis. Jibu sio mzuri sana hasa hasa msimu uliopita. Alifanya vibaya ukilinganisha na miaka miwili iliyopita.

2017-18, alisshuka kiwango chake cha ukabaji hadi kufikia asilimia 72 kutoka asilimia 89 kipindi akiwa na Mats Hummels in 2013-14. Sokratis wa sasa sio kama wa zamani. Labda umri nao unaenda.

Alilaumiwa sana kwenye mchezo wao dhidi ya Schalke waliokuwa wanaongoza mabao 4-0 lakini mwisho wa mchezo Mchezo ukaenda sare. Sokratis alikuwa akijiangusha hovuo kwa kudangaanya kaumia ili kupoteza muda, kabla ya kumfanyia madhambi Yevhen Konoplyanka, but rather na kusababisha bao.

Hajazeeka sana, Ni miaka 30 tu. Ngoja tuone kama Unai atafaulu na hesabu pia.

Na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here