Home Kimataifa “Vioja vya World Cup” Messi na Cr7 wavunja ndoa nchini Urusi

“Vioja vya World Cup” Messi na Cr7 wavunja ndoa nchini Urusi

9791
0
SHARE

Habari kutoka nchini Urusi zinasema wanandoa waliofahamika kwa majina ya Arsen na Lyudmila wamepeana talaka baada ya mabishano makubwa yaliyotokea kati yao kuhusu yupi bora kati ya Messi na Ronaldo.

Arsen ambaye ni raia wa Urusi alijikuta katika ugomvi mzito na Lyudmila ambaye ni mkewe baada ya kuanza kubishana, hali hii ilimlazimu Arsen kumpa talaka mkewe baada ya kuona anajibizana naye.

Mabishano hayo yalianza baada ya Arsen kushangilia kwa nguvu ushindi wa Argentina, ndipo mkewe akamponda kwa kumuambia Messi hamna kitu na hapo ndipo mambo yalianza kuharibika.

Arsen aliondoka nyumbani usiku huo na kesho yake alikwenda mahakamani katika mji wa Chelyabinsk katika mji wa Urals nchini humo kukamilisha talaka hiyo, Arsen na Lyudmila walikutana 2002 wakiwa baa wakiangalia kombe la dunia.

“Toka kombe la dunia linaanza alikuwa akimsema Messi akawa anasema hawezi kufunga hata penati, ilikuwa ikinikira sana alivyokuwa anamsifu Ronaldo nikaona ni bora tu tukae tofauti milele kwa kuwa hatuendani” alisema Arsen.

Messi alifanikiwa kuipeleka Argentina katika 16 bora lakini wakaondolewa na timu ya taifa ya Ufaransa, na siku hiyo hiyo Cristiano Ronaldo naye aliondolewa katika hatua hiyo na timu ya taifa Uruguay. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here