Home Kimataifa “Its Coming Home”, kwa mara ya kwanza Waingereza wanapeta kwa matuta

“Its Coming Home”, kwa mara ya kwanza Waingereza wanapeta kwa matuta

8133
0
SHARE

Bao la penati la dakika ya 57 la Harry Kane lilimfanya Kane kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi 6 mfululizo kwa Uingereza tangu Tommy Lawton kufanya hivyo kwa Uingereza mwaka 1939.

Bao la Kane lilionesha kama linaenda kuwapeleka Waingereza robo fainali ndani ya dakika 90 lakini katika dakika 5 za nyongeza beki wa timu ya taifa ya Colombia Yerry Mina aliipatia Colombia bao la kuongoza.

Goli la Yerry Mina linamfanya mlinzi huyo kufunga mabao 3 ya kichwa katika msimu huu wa kombe la dunia, na sasa anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao mengi ya kichwa tangu baada ya Miroslav Klose kufunga mabao mengi(5) ya kichwa 2005.

Baada ya dakika 90 kumalizika ilimfanya muamuzi kuongeza dakika nyingine 30, lakini hata 30 za ziada wakati zinamalizika bado matokeo yalikuwa ni yale yale ya bao 1-1.

Kimbembe kilianza baada ya muamuzi kusema sasa ni mikwaju ya penati, Waingereza wengi mitandaoni walionekana kuchanganyikiwa kutokana na rekodi yao mbovu ya penati na hata kabla hazijapigwa walishakata tamaa.

Lakini katika hatua ya matuta Uingereza walianza kukosa tuta lililopigwa na Jordan Henderson, lakini Colombia wenyewe Mateus Uribe na Bacca walikosa, wafungaji wa penati za Uingereza alikuwa Harry Kane, Marcus Rashford, Eric Dier na Tippier huku za Colombia zikiwekwa kimiani na Radamel Falcao, Juan Cuardado na Luis Muriel.

Golikipa wa timu ya taifa ya Uingereza Jordan Pickford anakuwa golikipa wa kwanza wa Uingereza kusave penati katika kombe la dunia tangu David Seaman kufanya hivyo mwaka 1998.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here