Home Kimataifa Inadaiwa Baba wa Obi Mikel alitekwa masaa machache kabla kuwavaa Argentina 

Inadaiwa Baba wa Obi Mikel alitekwa masaa machache kabla kuwavaa Argentina 

8824
0
SHARE

Tayari timu ya taifa ya Nigeria wameondolewa katika michuano ya kombe la dunia baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya taifa ya Argentina wakati wa hatua ya makundi.

Siku chache baada ya Nigeria kuondolewa, sasa kumeibuka habari mpya kwamba nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria Obi Mikel alipewa taarifa za baba yake kutekwa masaa machache kabla ya mchezo wao vs Argentina.

Obi alizipata habari hizp wakati yuko kwenye basi la timu kuelekea St Petersburg kuivaa Argentina na katika taarifa hiyo alionywa kwamba kama angeripoto tukio hilo mahala popote baasi angeuwawa.

Taarifa za tukio hilo alizipewa na mmoja wa watu wa familia yao aliyekuwa Nigeria ambapo anasema yeye alipigiwa simu na watekaji ambao walimuambia kuhusu jambo hilona kumtaka Obi alipe kiasi cha pesa.

Obi anasema baada ya tukio hilo kutokea aliamua kukaa kimya bila kumuambia mtu yeyote akiogopa kuwa kikwazo kwa wenzake kuelekea katika mchezo huo muhimu.

Baba mzazi wa kiungo huyo wa zamani wa Chelsea alitekwa wakati akielekea msibani katika eneo liitwalo Makurudi nchini humo kwa ajili ya msiba, ndipo watekaji walipotekeleza utekaji wao.

Baadae polisi walifanikiwa kumuokoa lakini alikutwa akiwa na majeraha mwilini mwake hali inayoonesha kupata mateso huko alikokuwa, hii sio mara ya kwanza kwa baba mzazi wa Obi kutekwa kwani August 2011 alifanyiwa tena tukio hili.

“Ninawashukuru maofisa wa usalama kwa kufanikiwa kumuokoa baba yangu na pia ninawashukuru watu wote wa karibu ambao walikuwa na mimi wakati napitia kipindi hiki kigumu” alisema Obi Mikel.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here