Home Kimataifa Hofu kubwa ya Waingereza iko hapa

Hofu kubwa ya Waingereza iko hapa

9387
0
SHARE

Tayari Wahispania wameondoka katika michuano ya kombe la dunia baada ya mikwaju ya penati dhidi ya timu ya taifa ya Urusi, hii ni moja kati ya matokeo ambayo yalizua taharuki zaidi kwa vigogo wa World Cup.

Hii leo Waingereza watakuwa Spartak Stadium kuwakabili Colombia, lakini kati ya kitu ambacho Gareth Southgate na vijana wake hawataki kukisikia baasi ni mikwaju ya penati.

Sio tu kwa wachezaji kama wachezaji lakini Southgate ni kati ya wachezaji wa zamani wa Uingereza ambaye amewahi kuigharimu Uingereza katika hatua ya matuta, hii ilikuwa 1996 katika nusu fainali ya michuano ya Euro.

Rekodi zinaonesha hakuna timu ya taifa yenye rekodi mbaya na mikwaju ya penati kama Three Lions, wakati Mexico na Romania wameshawahi kutolewa mara mbili mbili kwa mikwaju ya penati, Waingereza wenyewe qametolewa mara tatu.

1990 waliondolewa na Ujerumani Magharibi, Argentina wakaja wakawatoa mwaka 1998 na baadae Ureno mwaka 2006 huku rekodi hii mbovu ikiwaua pia Ulaya ambako walitolewa mara 3/4 katika michuano hiyo kwa tuta.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na hata mlinda lango wao hawana uzoefu linapokuja suala la matuta kwani pia wachezaji wengi wa Uingereza sio wapigaji wa penati katika timu zao.

Uwepo wa Harry Kane na Jamie Vardy unawapa matumaini kiasi flani Waingereza kuhusu penati lakini tayari Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekosa penati katika michuano hii na inaleta hofu kwa wachezaji wakubwa kupiga tuta.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here