Home Kimataifa Brazil vs Mexico, takwimu muhimu kuelekea vita hii ya America

Brazil vs Mexico, takwimu muhimu kuelekea vita hii ya America

8125
0
SHARE

Leo ndio leo ambapo timu inayopendwa zaidi na Waafrika Brazil itakuwa kibaruani dhidi ya moja ya timu tishio sana katika michuano hii Mexico, huku mchezo wa leo atakayefungwa anarudi nyumbani.

Brazil wanaweza kumkosa Marcelo aliyeumia katika mchezo uliopita na japokuwa jana alifanya mazoezi ila anaweza kuanzia benchi, Mexico wenyewe watamkosa mlinzi wao Hector Moreno ambaye anatumikia adhabu ya kadi.

Katika rekodi Wabrazil wanaonekana wazuri sana mbele ya Mexico kwani katika michezo minne iliyopita, Mexico hawajawahi kupata ushindi kwa Brazil na hata kufunga goli(wamefungwa 3 na suluhu 1).

Lakini pia katika michuano ya kombe la dunia, timu ya taifa ya Brazil haijawahi kupoteza mchezo dhidi ya timu inayotokea ukanda wa Marekani ya Kaskazini au ya kati.

Katika fainali 6 za kombe la dunia zilizopita, timu ambazo zilikuwa zikiifunga Brazil zilikuwa ni za kutokea Ulaya na mara ya mwisho Brazil kufungwa na timu ambayo haitokei Ulaya ilikuwa 1990 walifungwa na Argentina.

Kama hii leo Brazil itawaondoa Mexico katika michuano hiyo baasi itakuwa mara ya 6 mfululizo kwa timu ya taifa ya Mexico kuondolewa katika hatua ya 16 bora.

Ushindi pekee kwa Mexico dhidi ya timu zinazotokea bara la America Kusini katika kombe la dunia ilikuwa mwaka 2002 ambapo Mexico waliifunga Ecuador kwa mabao 2-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here