Home Uncategorized Ubelgiji wavunja rekodi iliyodumu miaka 52, sasa kuwavaa Brazil robo fainali

Ubelgiji wavunja rekodi iliyodumu miaka 52, sasa kuwavaa Brazil robo fainali

9567
0
SHARE

Inaweza kuwa mecho bora kabisa ya kombe la dunia, hii ni baada ya Ubelgiji kutoka nyuma ya mabao 2 kwa 0 na kisha kuibuka na ushindi wa bao 3-2 katika mechi yao ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani.

Kipindi cha kwanza kiliisha bila bao lakini kipindi cha pili Genki Haraguchi 48′ na Takashi Inui 52′ waliitanguliza Japan kabla ya Jan Vertonghen 69′ na Marouane Fellaini 74′ kufanya matokeo kuwa 2-2, lakini dakika ya 90 Nacer Chadli aliimaliza Japan.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya taifa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kwenda kuibuka na ushindi tangu Uingereza wafanye tukio kama hilo katika michuno hiyo mwaka 1966 dhidi ya timu ya taifa Korea(ndani ya dakika 90).

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo Ubelgiji waligusa mpira mara 26 katika lango la timu ya wapinzani, hii ni mara ya kwanza katika michuano ya mwaka 2018 kwa timu moja kugusa mipira mara nyingi katika box la wapinzani.

Katika mchezo wa leo kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez alifanya mabadiliko 10 na haya yakiwa mabadiliko mengi zaidi katika kombe la dunia tangu Saudi Arabia wafanye mabadiliko 11 ya kikosi cha kwanza mwaka 2006.

Baada ya matokeo ya Ubelgiji na ushindi wa timu ya taifa ya Brazil sasa tunakwenda kuona robo fainali kati ya miamba miwili iliyotabiriwa kushinda kombe la dunia msimu huu ni Brazil vs Ubelgiji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here