Home Kimataifa RUS 2018: VAR inamjua Neymar na Shaffih anapajua Samara

RUS 2018: VAR inamjua Neymar na Shaffih anapajua Samara

11900
0
SHARE

The champions are Come back! Mliosoma English Medium nisaidieni hapo kama nipo sawa. Hata hivyo hayo sio maneno yangu, ni maneno ya mashabiki wa Brazil waliokuwa wakishangilia ushindi wao. Hatimaye Mexico wataungana na Akina Messi na Ronaldo kurudi kwao. Mabao ya Roberto Firmino na Neymar. Mchezo huu umechezwa jijini Samara.

Kama tunavyojua Urusi ni nchi inayotengeneza vyombo sana. Nikimaanisha pombe. Inaonekana Wabrazil baada ya kutoa dozi hii wataenda kupiga vyombo.

Shaffih dauda nae leo alikuwepo Samara. Sina uhakika sana na hali yake huko Samara kama nae ameungana na wabrazil kwenda kupiga vyombo au lah (Natania).

Huu mji wanatengeneza kinywaji kinachojulikana kama Zhigulyovskoye. Huu mji wakati wa vita vya pili vya dunia serikali ya Urusi zamani kama Soviet ilikimbilia kwenye jiji hili ambapo zamani ulijulikana kama Kuibyshev baada ya mji wa Moscow kuvamiwa na wajerumani.

Mapema kabla ya mtanange huu Wabrazil wengi walionekana kwenye boti mbali mblali ambapo zilikuwa zinapita kando kando ya mto Volga. Mji huu umezungukwa na mto Volga River. Wabrazil wanapenda raha sana hivyo mazingira ya mji huu yamewakumbusha kule Copa cabanna.

Mapema hivi leo Dauda anasema mji huu ni mji wa kihistoria. Ni mji ambao Roketi maarufu za Urusi zimetengenezwa. Ni miongoni mwa miji 11 unaoandaa michuano ya kombe la dunia. Michezo 6 ya hatua ya makundi na michezo minne ya hatua ya mtoano ukiwezo mchezo wa Urusi na Hispania na ule wa Brazil dhidi ya Mexico.

Katika mchezo wa leo tumeona Neymar akigharagara chini kwa kudai kuwa amekanyagwam Ni kweli amekanyagwa lakini sio kwa kukirusha kule. VAR yenye we imeshamjulia Neymar ni mchezaji wa aina gani ndio maana wamempuuza ili ajikaze kiume.

Nikamuuliza vipi kuhusu historia ya uwanja huu.

“Huu ni uwanja ni mzuri sana lakini hapo awali ulikumbwa na sintofahamu ambayo ingepelekea kutokuruhusiwa kutumika!

Kwanini?

“Uwanja huu ulitengenezwa kwa ajili ya kombe la dunia tu. Una uwezo wa kubeba mashabiki 45,000. Uwanja huu ulichelewa kukamilika jambo lililopelekea FIFA kujaribu kuingilia kati, uwanja huu umetengenezwa upya kabisa kama nilivyosema awali, na umetengenezwa takribani kilometa7 nje ya mji wa Samara.

Hata hivyo watu wengi hasa hasa watanzania wameshindwa kufika katika uwanja huu kutokana na umbali na gharama nyingi.

Muonekano wa mji huu umekaaje

“Mji huo ni mji wa viwanda. Pilika pilika nyingi za mji huu umetulia kiasi kwamba sauti za viwanda ndizo zinazosikika zaidi”

Vipi hali ya Mashabiki?

Mashabiki wengi waliojaa mpambano wa Brazil dhidi ya Mexico, Mashabiki 42 wametoka amerika wote ila mashabiki 3000 ndio sisi wengine wa changanyikeni. Brazil wameujaza zaidi uwanja huu. Dauda anasema kila mshabiki aliyeko pembeni yake anaonekana kama kuchanganyikiwa. Huu ni mchezo wa 42 timu hizi kukutana. Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hizi kukutana kombe la dunia Mexico hawajafanikiwa kupata bao hata moja.

Swali lingine la kujiuliza ni, Je? Gabriel anampa nini Titte? Gabriel ni mchezaji pekee tokea 1998 ina mchezaji annayevaa jezi namba 9 amecheza michezo minne ya kombe la dunia bila bao. Roberto Firmino ameingia dakika kadhaa tu na ameonesha kuwa yeye ndiye aliyepaswa kuvaa jezi namba 9.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here