Home World Cup RUS 2018: Shkamoo Kagawa, Fellain anawasalimia

RUS 2018: Shkamoo Kagawa, Fellain anawasalimia

9851
0
SHARE

Kama hujapata burudani kombe la dunia la mwaka huu, ndugu yangu nadhani furaha pekee utakayopata ni siku utakabidhiwa tiketi ya mbinguni. Kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia, wachezaji wawili waakiba wanaingia uwanjani na kufunga mabao mawili.

Nimeshindwa kuelewa hili ni kombe la dunia au vita ya dunia!!!!! Hakuna timu ndogo hakuna timu kubwa. Ubelgiji wanapelekwa mchaka mchaka na timu ambayo haijawahi kufuzu hatua ya Robo fainali? Taifa Stars tujipange 2022 huenda na sisi tukafanya maajabu.

Nilichofurahishwa nacho leo ni kwa namna wale wachezaji ambao dizaini fulani kama wamesuswa hivi, au walionekana hawafai, au hawakubaliki, walivyotoa burudani mubashara kwa kuwanyanyasa wale tunaonwaona bora. Shinji Kagawa ametawala dimba lote utadhani Kelvin de bruyne amelewa mbege. Fellain asiyependwa na mashabiki wengi wa Man United leo katuma salamu kwa wale mashabiki wenzangu na mimi waliochukizwa na taarifa za yeye kuongeza mkataba wa miaka miwili. Nacer Chadli 2016 Spurs walimwambia aondoke tu. Leo hii hakuna cha Hazard wala bibi yake Lukaku, Ubelgiji nzima itakuwa ni Chadli tu.

Rekodi iliyowekwa usiku wa leo hii ni kwa mara ya kwanza timu inatoka nyuma kwa mabao mawili na kusinda mchezo ndani ya dakika 90 tokea mwaka 1966 Ureno ilipoifunga Jamhuri ya Korea mabao 5-3 .

Huyu Chaldi huyu aliyeichezea Morocco mwaka mmoja kabla ya kuhama utaifa nani aliyemshauri kufanya hivyo? ametumia sekunde nane za mwisho kumaliza uhai wa wajapan. Katika mchezo wa leo Genk Haraguchi anakuwa mchezaji wa kwanza wa Japan kufunga bao la kwanza katika hatua ya mtoano ya kombe la dunia.

Wakati natoka kwenye banda nikakutana na jamaa mmoja akaniuliza “Hivvi mechi ijayo ni Brazil na Ubelgiji sio? Mshkaji mwingine akadakia akasema haoa, Ni ubelgiji na Brazil! Sasa nimeshindwa kuelewa kwamba timu inayoanza kutajwa ndio bora au vipi!

Baada ya mchezo nimewaza sana. Japan wanamiliki mpira kwa asilimia 42? Mbele ya Witsel, Hazard na De bruyne? Kivipi? yaani inakuwaje? inawezekana vipi Japan kupiga mashuti 11 mbele ya Vertogen na Tobby? Daaah hapana aiseee.! Niamini mimi! ukisikia mtu anakwambia eti Bingwa wa kombe la dunia mwaka huu ni fulani, basi wala usijibizane nae huyo mtu maana nina uhakika hafuatilii kombe la dunia. Japan wamevunja rekodi yao ya kufunga mabo mengi katika kombe la dunia kwa kufunga mabao 6.

Niliongea na kapombe wa Simba. Akaniambia hajui bingwa ni nani! Nikamuuliza swali hilo hilo Madee! Madee akasema yeye mwenyewe amebaki njia panda!

Jamaa mmoja akanitumia meseji akaniambia endapo Colombia atamfunga Uingereza kesho basi hili litakuwa kombe la dunia bora kuwahi kutokea. Sijajua kamaanisha nini. Mwingine akaniambia timu ikiwa na wachezaji wa Man U raha sana. Mashabiki wa Man u mna nini lakini?

Mtazamo wangu kuhusu mchezo wa leo

Kosa la mchezo wa leo ni la Martinez mwenyewe. Kwanza amewadharau sana Japan. Amecheza bila kujihami. Amecheza kwa kushambulia zaidi. Timu nzima aliipeleka mbele. Ubelgiji walifanikiwa kugusa mpira mara 26 kwenye nusu ya uwanja upande wa Japan kipindi cha kwanza lakini wakafanikiwa kupiga mashuti mawili tu.

Kuna wakati ukiangalia safu ya ulinzi ya Ubelgiji walikuwa wanashindwa kabisa kuhamisha mpira kutoka eneo lao baada ya kiungo mchezeshaji kupotezwa na kagawa. Kagawa alitawala dimba kwa sababu kubwa kwamba hakukuwa na kiungo mkabaji aliyemsumbua.

Moja ya vitu vinanipa wasiwasi ni safu ya ulinzi ya Ubelgiji. Ni mbovu kiasi kwamba nashindwa kuelewa wamechoshwa na nini haswa. Na ubovu huu unaenezwa zaidi na mfumo wa mabeki watatu ambao Martinez anapenda kuutumia. Kuna kila sababu ya mchezo ujao Martinez akabadili mfumo la sivyo huo utakuwa mwisho wa safari yao.

Awamu hii ni mwendo wa kuhamahama timu mpaka pale mtu utakapopata kombe la dunia.

Licha ya kufungwa, Mashabiki wa Japan moja ya jambo la kisoka waliloonesha ni pale kijana mdogo alipoonekana akisafisha uwanja mara baada ya mchezo huo kukamilika. Ingekuwa hapa bongo kwetu wengine ndo kwanza wamgewaza kuvunja viti

Na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here