Home World Cup RUS 2018: Fahamu namba hizi walizoondoka nazo Hispania

RUS 2018: Fahamu namba hizi walizoondoka nazo Hispania

8440
0
SHARE

1056

Spain wamekamilisha pasi 1056 ndani ya dakika 120 za mchezo wao wa mwisho dhidi ya Urusi. Katika dakika 90 za mchezo walifanikiwa kugusa mpira mara 1013. Kimahesabu hapo ndani ya dakika 30 za nyongeza waligusa mpira mara 43 tu. Kimahesabu kama wangepiga pasi 43 kila baada ya dakika 30 wangepiga pasi 138 tu. cha ajabu wamepiga zaidi ya 1000 na wamepata bao moja tu. Juzi nilitazama bao la Cavan dhidi ya Ureno zilipigwa pasi mbili, kutoka kwa kipa kisha kwa aliyetoa asisti kabla ya Cavan kuweka wavuni.

Hii ni mara ya 4 timu inacheza zaidi ya pasi 1000 ndani ya dakika 90 tokea mwaka 1966 . Brazil pia walifanya hivyo (vs Italy 1994), Spain (vs Germany 2010) na Germany (vs Algeria in 2014).

48

Russia kwa mara yao ya kwanza kabisa wanaingia katika hatua ya robo fainali ndani ya miaka 48 iliyopita. Mara yao ya mwissho ilikuwa kule nchini Mexico mwaka 1970 walipokuwa wakijulikana kama Soviet Union. Ilikuwa mara yao ya kwanza kwenda kwenye mikwaju ya penati katika kombe la dunia huku Hispania ikiwa mara yao ya 4. Argentina ndio wenye idadi kubwa ya kuingia mikwaju ya penati katika kombe la dunia nayo ikiwa ni mara 5.

431

Spain hawajahi kuruhusu bao lolote World Cup kwenye hatua yoyote ya mtoano kwa muda wa dakika 431. Mara yao ya mwisho kuruhusu bao ilikuwa hatua ya 16 bora dhidi ya France mwaka 2006, Zinedine Zidane alipoisaidia timu yake kupata ushindi dakika za lala salama 3-1.

3

Spain inakuwa timu ya tatu kukosa ushindi kwenye mikwaju ya penati wakiwa na England pamoja na Italy mara tatu kwenye historia ya kombe la dunia. Walipoteza kwa Belgium mwaka 1986 na South Korea mwaka 2002, na zote kwenye robo fainali.

1, 7, 6

De gea ameokoa mchomo mmoja kati ya mashuti 7 aliyopigiwa na kufungwa mabao 6. Usisahau alipigwa Hat trick na Ronaldo

5

Spain sasa wameweka rekodi ya kucheza na mwenyeji mara tano katika kombe la dunia, kabla ya Russia, alicheza na South Korea , Hispania walipoteza mikwaju ya 5-3 mwaka 2002. Wamecheza na Italy (mara mbili mwaka 1934) pia walikutana na Brazil (1950) na hawajawahi kufanikiwa kupata ushindi kwa mwemyeji yoyote yule.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here