Home Kimataifa Neymar akaa juu ya Messi na Cr7 Brazil wakienda robo fainali

Neymar akaa juu ya Messi na Cr7 Brazil wakienda robo fainali

8758
0
SHARE

Rekodi mbovu ya Mexico mbele ya timu ya taifa ya Brazil imeendelea tena hii leo baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Brazil na sasa Mexico wanakuwa wamecheza mechi 5 dhidi ya Brazil bila ushindi.

Goli la Neymar 51′, Ilimchukua Cristiano Ronaldo mashuti 74 kufunga mabao 6 katika timu ya taifa na ikamchukua Messi mashuti 67 kufunga goli kombe la dunia, lakini mashuti ya Neymar 38 tu yanamfanya kufikisha mabao 6.

Baada ya bao la Neymar sasa anakuwa amewazidi Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika mabao ya hatua ya mtoano kwani Neymar sasa anakuwa ana bao moja huku Messi na Ronaldo wakiwa hawajawahi kufunga katika hatua hii.

Bao hili pia linamfanya Neymar kufikisha jumla ya mabao 57 kwa Brazil katika mechi 89 huku akiwa na umri wa miala 26 tu na pia anakuwa amefunga mabao 15 katika mechi 16 alizoichezea PSG na Brazil kwa mwaka 2018.

Bao la pili la Brazil lilifungwa na Roberto Firminho dakika ya 88 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Neymar inayomfanya Neymar sasa kutengeneza jumla ya nafasi 16 za mabao katika mashindano haya.

Matokeo ya hii leo yanaifanya Mexico kutolewa katika hatua ya 16 bora kwa mara 6 mfululizo katika michuano hii(1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014 na 2018), huku Rafael Marquez akivunja rekodi ya Stanley Mathews kuwa mchezaji mzee kuwahi kuanza katika mecho ya mtoano World Cup.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here