Home Kimataifa Mexico na deni la magoli 11-0 vs Brazil – Leo watalipa kisasi...

Mexico na deni la magoli 11-0 vs Brazil – Leo watalipa kisasi au uteja kuendelea?

9428
0
SHARE

Mission ya Brazil kufuta makosa yao yao ya kuondolewa kwa aibu kwenye michuano ya 2014 FIFA World Cup inaendelea baada ya kufuzu kutoka kwenye kundi E wakiwa na pointi 7, sare moja ba ushindi mara 2.

Mexico baada ya kuanza kwa soka la kuvutia na ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa 2014, Ujerumani – wakashinda tena vs Korea, kisha wakamaliza na kipigo kizito cha 3-0 ambacho kingeweza kuwaondoa kwenye mashindano dhidi ya Sweden. Leo wanaingia kwenye mchezo wakiwa wametoka kunusurika kwenye ndoto la Sindano – wanakutana na timu ambayo walitoka nayo sare katika mchezo wa mwisho waliokutana nchini Brazil 2014 – mechi hiyo iliisha kwa sare tasa – ikiwa ni mechi pekee kati ya 4 ambazo Brazil walikutana na El Tri na kushindwa kupata ushindi.

Vikosi: 🇧🇷 Felipe Luis ataanza badala ya Marcelo ambaye alishindwa kuendelea na mchezo dhidi ya Serbia kutokana na majeruhi ya mgongo.

Marcelo alifanya mazoezi jana na huenda akawepo kwenye benchi.

Danilo amepona majeraha ya paja ambayo yalimweka nje katika mechi vs Serbia lakini mbadala wake Fagner huenda akaendelea kucheza.

Mexico 🇲🇽 watakuwa na pengo la beki wa kati Hector Moreno, ambaye amefungiwa kutoka na kadi mbili za njano. Hugo Ayala atachukua nafasi yake.

Takwimu:

•Brazil hawajapoteza mchezo wowote kati ya minne waliyokutana na Mexico katika kombe la dunia – wameshinda 3 na sare 1. Brazil hawajaruhusu goli hata moja katika mechi hizi – wakiwa na ushindi wa jumla wa 11-0

•Mchezo wa mwisho wa kombe la dunia ulikuwa 2014, uliisha kwa sare ya 0-0, tangu wakati wamekutana ten katika mchezo wa kirafiki wa ushindi wa 2-0 jijini Sao Paulo June 2015 magoli ya Philippe Coutinho na Diego Tardelli.

Brazil 🇧🇷

•Brazil hawajawahi kupoteza mechi ya World Cup dhidi ya timu ya Amerika ya Kaskazini wala ya kati.

•Mechi zao 6 za mwisho kufungwa katika World Cup zilikuwa dhidi ya mataifa ya ulaya tu. Timu ya mwisho kuifunga Brazil ya ambayo haitoki bara la ulaya ilikuwa Argentina mwaka 1990, katika hatua ya 16 bora kwa goli la Claudio Caniggia.

Mwaka 1990 ndio mwaka wa mwisho wa Brazil kushindwa kufika hatua ya robo fainali ya World Cup

▪ Katika mechi 8 zilizopita wamepata clean sheet 7 – wakishinda mechi 6 na sare 2.

Mexico 🇲🇽

▪ Ushindi pekee wa Mexico katika World Cup vs timu kutoka Amerika ya Kusini ulikuwa dhidi ya Ecuador katika hatua ya makundi mwaka 2002 ambapo walishinda 2-0.

▪ Endapo watafungwa Mexico watakuwa wametolewa kwenye raundi ya 16 bora ya World kwa mara 7 mfululizo.

▪ Mara ya mwisho wamefika hatua ya robo fainali ya World Cup ilikuwa mwaka 1982 walipowafunga Bulgaria 2-0 na kwenda robo kutolewa na Ujerumani Magharibi.

▪Huu utakuwa mchezo namba 57 wa kombe la dunia kwa vijana wa kutoka Sinaloa – idadi kubwa kuliko timu yoyote ile ambayo haijawahi kutwaa kombe hili.

.:

Je Mexico wataandika historia mpya leo?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here