Home World Cup RUS 2018: Je Yusuf wa Tanga atampeleka Modric nyumbani?

RUS 2018: Je Yusuf wa Tanga atampeleka Modric nyumbani?

7672
0
SHARE

Leo ndio leo. Wasambaa na wadigo wote imoo. Ni mtanange wa kufa au kupona. Huu utakuwa na mchezo wa hatua ya mtoano utawakutanisha Croatia, dhidi ya Denmark. Mchezo huo utapigwa Katika dimba la Nizhny Novgorod, saa tatu kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki ya kati.

Croatia wamemaliza katika kundi lao wakiwa kileleni na alama tisa mkononi.

Kuelekea mchezo wao tunatarajia kuwaona wachezaji wote ambapo mchezo wao dhidi ya Iceland, walipumzishwa. Hakuna taarifa zozote kwa Croatia kuhusu majeruhi.

Kocha wa timu ya taifa Croatia, Zlatko Dalic, amesema
“Presha yetu kubwa zaidi inataka ushindi. kwenye hatua ya makundi tumevuna kitu kizuri na imetupa kujiamini zaidi,”

“tunajua haitokuwa rahisi kwetu wapinzani wetu wamejipanga, tunahitaji kujituma ili tupate ushindi,”

Wananchi wote wa mkoa wa Tanga tunaoenda kuwaatarifu kuwa Yussufu Poulsen leo atakuwepo. Tunapenda kuwaambia wasambaa wote kwamba Poulsen anategemewa kurudi katika kikosi baada ya kuwa nje akitumikia adhabu ya kadi ya njano.

Tukiachana na wasambaa pia Denmark wanatwgemea kiungo wao wa kati William Kuvist, ambaye alikuwa anaumwa mbavu kurudi katika mchezo huu.

Kocha wa timu ya taifa Denmark, Age Hareide, akiongelea mchezo wao dhidi ya Croatia
“nafikiri utaona mabadiliko kutoka kwa Denmark, unahitaji kuona mpira tunaocheza tunahitaji kukaba na kushambulia, inawezekana kuwa mechi ya watu wawili Modric, na Eriksen, inaweza kuvutia zaidi,”

Kumbukumbu.
Croatia, na Denmark, wamekutana mara sita. Denmark, wamefika hatua ya mtoano mara nne. Magoli sita ya Croatia, yamefungwa kipindi cha pili.

Mimi Nabeti Croatia anatoka.

Habari na Aziz Mtambo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here