Home World Cup RUS 2018: Brazil kwa Ubelgiji? Watakiona cha mtemakuni

RUS 2018: Brazil kwa Ubelgiji? Watakiona cha mtemakuni

8931
3
SHARE

Kwa mtazamo wangu kuna uwezekano mkubwa Ublegiji wakatushangaza. Wachezaji wake wengi wana morali kubwa.
Nimesikiliza mahojiano ya Kelvin na nimetazama na baadhi picha alizoweka kwenye kurasa zake (Upande wa stori Instagram). Kdb anasema

Mwaka 2013, Niliambiwa nikae benchi nisubiri muda wangu. Hapa alimaanisha Jose Mourinho

Mwaka 2014, Nikaenda Ujerumani watu wakasema nimepoteana. Hapa akiwalenga waandishi wa habari.

Mwaka 2016 nikarudi England watu wakasema nimefanya makosa mziki wa England siuwezi Nitafeli. Pia aliwalenga wale mashabiki waliokuwa kinyume na Man City

Mwaka 2017 wakasema sina uwezo wa kulibeba taifa langu. Hapa aliwalenga watu walioibeza Ubelgiji kwamba haiwezi kufanya vziru

Ukijaribu kuangalia hizi kauli zake utagundua anawalenga wale wote wenye chuki dhidi yake au wale waliojaribu kukwamisha jitihada zake.

Kelvin pia anaamini kuwa zipo changamoto nyingi katika juhudi za kutimiza ndoto zake kitimu. Ubelgiji ni moja ya timu hatari zaidi licha ya kwamba watu wameipa nafasi kiduchu sana.

Kelvin pia anasema kuwa yeye sio kwamba ana kiburi lakini anaamini kwamba ili uwe mchezaji mzuri ni lazima usikilize ushauri wa watu wengine, lakini wachezaji wakubwa hufanya maamuzi yao wenyewe. Haamini kwamba lazima wakubalike na kila mtu ili wao wafanye vizuri lakini wao wanaweza kufanya makubwa na watu wakaanza kuwakubali.

Ukiangalia kwa Makini utagundua Kelvin ana imani kubwa ndani yake ambayo inaleta hamasa kwa timu.

Ubelgiji ina timu hatari zaidi tofauti na watu wengi wanavyoitizamia. Mimi nina imani ukiwa na Hazard mwenye mabao 69 na asisti 46 kwenye michezo 208 ya ligi kuu England, huku Ligi ya ufaransa akiwa na mabao 21 na asisti 41 kwenye michezo 107, akisaidiana Kdb mwenye asisti 46 za ligi kuu England na mabao 21 kwenye michezo 101, huku Bundasliga akiwa na asisti 36, na mabao 23 katika michezo 85, kwa watu hawa na kwa uwezo mkubwa walio nao hasa hasa wa kucheza kitimu basi una uhakika wa kuifunga timu yoyote. Tena mbaya zaidi ukiwa una washambuliaji wawili hatari kabisa Romelu Lukaku mwenye magoli 51 kwenye michezo 85 ndani ya miaka miwili na Dries Martens mwenyewe magoli 56 kwenye michezo 96 ndani ya miaka miwili pia unataka nini cha ziada?. Maanake hapo una washambuliaji wenye magoli 107.

Ndugu yangu kama Brazil watafanikiwa kuvuka wakikutana na hawa jamaa wajiandae kisaikolojia.

Mimi nilikuwa shabiki namba Moja wa Brazil lakini kwa sasa nahamisha mawazo yangu. Kama Brazil watafanikiwa kuwatoa Mexico halafu wakakutana na hawa wanaume utakuwa mchezo ambao utavutia zaidi lakini Brazil watakiona cha mtemakuni

Comments

comments

3 COMMENTS

  1. Belgium mbele wa nawashambuliaji watatu hatari hazard tunampa Miranda lukaku tunampa Silva na Batman au batshuai huyo unajua atakua na kisiki Marcelo alaf Belgium ukimzibiti Kelvin de Bruno inamaanisha hazard,lukaku na batman amna magoli as washambuliaji wa Brazilian watazuiwa na nani ukimzuia neymar continho anakutoboa ukimzuia conti casemiro anakukaza bado Jesus fiminyo wrote hao ni wakazaji pole mkuu tutashuhudia fainali na yyte hatakaye pita ndo bingwa

  2. Comment:Mwenyej Hofu kua Brazil itatolea na Belgium bac hana tofauti na Petro alie mkana Yesu,Nyote mtarudi 2 kundini….Njr taratbu fomu na makar yamerud. Alikua nje ya pitch for 3 months na bado ni hatarii Asee.,#Brazil ndie Bingwa na ubelgiji itatolewa na yule yule STAR man NEYMAR Jr

Leave a Reply to Khalid Cancel reply

Please enter your comment!
Please enter your name here