Home Kimataifa Matuta yawarudisha nyumbani De Gea na Dermark

Matuta yawarudisha nyumbani De Gea na Dermark

7922
0
SHARE

Michuano ya kombe la dunia imepigwa tena hii leo na kama ilivyokuwa jana, kigogo mwingine ameanguka leo. Ni mabingwa wa michuano hiyo Hispania ambao wameondolewa na wenyeji wa kombe la dunia timu ya taifa Urusi.

Hispania 1(penati 3) – Urusi 1(penati 4). Ushindi wa penati 4-3 sasa unayafanya mataifa matano wenyeji wa michuano hii kushinda kwa penati mfululizo katika hatua ya mtoano, Ufaransa 1998, Korea 2002, Germany 2006, Brazil 2010.

Bao ambalo hii leo Hispania walilipata lilitokana na mpira wa kujifunga, goli hili linaifanya Urusi kuwa timu ya pili kuwahi kujifunga mara mbili katika msimu mmoja wa kombe la dunia baada ya Bulgaria 1966.

Croatia 1(penati 3) – Dernamark 1(penati 2). Bao la sekunde ya 57 la Mathias Jorgensens linakuwa bao la pili kufungwa mapema katika kombe la dunia baa ya goli la Clint Dempsey aliyetumia sekunde 29 mwaka 2014.

Mchezo wa leo unakuwa mchezo wa pili katika historia ya michuano ya kombe la dunia ambao timu zote zinafunga goli chini ya dakika 4, mara ya mwisho hii ilitokea mwaka 2014 katika mechi kati ya Argetina vs Nigeria.

Hii leo inakuwa mara ya pili katika historia ya kombe la dunia kwa mechi mbili kuamuliwa kwa penati, tukio kama hili lilijitokeza mara ya mwisho katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1986.

Kwa matokeo ya hii leo sasa Hispania wanaunga na Argentina na Ureno katika safari ya kurudi makwao huku Urusi wenyewe na Croatia wakiendelea kupeperusha bendera Urusi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here