Home Kimataifa RUS 2018: Takwimu za Messi na Ronaldo kombe la dunia.

RUS 2018: Takwimu za Messi na Ronaldo kombe la dunia.

10625
0
SHARE

Kwanza kabla hatuaongelea kuhusu Messi na Ronaldo ambao watani humuita mmoja Kirikuu na mwenzake Penaldo acha nikupe KIFURUSHI.

Kwa Mara ya pili Bingwa wa Ballon d’Or anatolewa na timu kutoka Bara la Amerika. Mwaka 2001 Michael Owen alitwaa tuzo ya Ballon d’Or. Mwaka 2002 Brazil wakakutana na Uingereza. Uingereza ikafungwa mabao 2-1.

Mwaka jana Cristiano Ronaldo alibeba BDO, kisha mwaka huu anafungwa na Uruguay Mabao 2-1 akiwa mtetezi wa Ballon d’Or.

Mwaka huu Uruguay imeitoa timu inayotoka nje ya bara la Amerika katika hatua ya 16 bora kwa mabao 2-1 ikiwafunga Ureno. Mabao yote yakifungwa na mchezaji mmoja (Edson Cavan). Rekodi hii pia inafanana na ile ya mwaka 2010 ambapo waliifunga timu inayotoka nje ya bara la Amerika kwa mabao 2-1 dhidi ya Korea kusini yote yakifungwa na mcheza mmoja (Luis Suarez).

Hii ni kwa mara ya tatu Uruguay wanamaliza hatua ya makundi wakiwa hawajaruhusu bao lolote. Mwaka 1930 na mwaka 1954. Pia hii ni kwa mara yao ya 3 inafanikiwa kuitoa timu kutoka ulaya katika hatua ya 16, Mwaka 1954 waliitoa Urusi kwa mabao 1-0 na Walifanikiwa pia kuwafunga Ujerumani Magharibia mabao 4-2.

Messi na Ronaldo wote out katika hatua ya 16 bora. Argentina imeshindwa kuvuka hatua ya 16 bora mara mbili 1994 na 2018 sawa sawa na Ureno ambao nao wameshindwa kuvuka hatua ya 16 bora mara mbili na zote wakiwa na Cristiano Ronaldo mwaka 2018 na 2010.

Messi ana miaka 31 na Ronaldo ana miaka 34. Wote kwa sasa ni manahodha wa timu zao za taifa. Wote wameanza kucheza kombe la dunia mwaka 2006. Wote walibahatika kufunga bao 1-1 kwenye fainali zao za kwanza.

Michuano Lionel Messi Cristiano Ronaldo
Brazil 2014
Mabao 4 1
Asisti 1 1
Michezo 7 3
South Africa 2010
Mabao 0 1
Asisti 1 1
Michezo 5 4
Germany 2006
Mabao 1 1
Asisti 1 0
Michezo 3 6
Urusi 2018
Mabao 1 4
Asisti 2 0
Michezo 4 4
Jumla
Magoli 6 7
Asisti 5 2
Michezo 19 17

Hizo ni takwimu za Makombe ya dunia yaliyopita. Kila mmoja ana tafsiri yake moyoni kwamba yupi aliyebora. Vijana wawili kwa klabua ya PSG Cavan na Mbappe wamehitisha kombe la dunia la Messi na Ronaldo kwa mwaka huu. Ronaldo amesema kwamba yupo tayari kucheza soka mpaka atakapotimiza miaka 41. Messi alipoulizwa kuhusu kuendelea kubakia timu ya taifa alisema inategemea timu yake ya taifa inafikia wapi.

 

Messi amewahi kufika fainali na Ronaldo bado hajaonja utamu wake. Messi amewahi kucheza kombe la dunia bila kufunga bao lolote. Ronaldo hajawahi. Messi na Ronaldo mwaka huu wote wamekosa penati katika fainali hizi.

Najua una stresi, Kwa leo niishie hapa. Nisiseme zaidi. Naitwa Privaldinho nipo Instagram pia waweza kunifollow.

Pia Kama upo Dar njoo tukutane Escape one kesho mapemaa saa 11. Soka la kulevya na dstv pamoja na bia ya kilimanjaro lager.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here