Home Kimataifa PSG yawazima Cr7 na Lionel Messi, sasa kazi kwa Neymar

PSG yawazima Cr7 na Lionel Messi, sasa kazi kwa Neymar

9630
0
SHARE

Washambuliaji wawili wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa Kylian Mbappe pamoja na Edison Cavanni wamewatoa nje ya michuano ya kombe la dunia nyota wawili wakubwa zaidi katika soka kwa sasa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Ufaransa 4 – Argentina 3. Kylian Mbappe alifunga mabao 2 na sasa anakuwa kinda wa kwanza U-20 kufunga mabao 2 katika mechi moja ya kombe la dunia tangu Pele afanye hivyo 1958.

Lionel Messi alitoa assist mbili ambazo kwa sasa zinamfanya kuwa Muargentina wa kwanza kupiga assist mbili kwenye kombe la dunia tangu Diego Maradona afanye hivyo katika kombe la dunia 1986 vs Korea.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kikosi cha Argentina, ni mara yao ya kwanza wanafunga mabao 3 katika mechi moja lakini wanaondoka bila ushindi.

Uruguay 2 – Ureno 1. Kuanzia mwaka 1966 ni Grezegorz Lato na Andrzej Szarmach(mabao 5 Poland) na Michael Ballack/Miroslav Klose(5 Ujerumani) ndio pacha pekee zenye mabao kuliko Edison Cavanni na Luis Suarez(4).

Wakati mashabiki wa Cr7 wakimponda Messi lakini kwa taarifa tu ni kwamba kipindi cha kwanza Cr7 aligusa mpira mara 24 tu na mara zote hizp hakuna aliyogusa katika eneo la box la wapinzani.

Baada ya kutolewa wote wawili hii leo sasa ina maana Cr7 na Messi wote hawajawahi kufunga goli katika hatua ya mtoano, Ronaldo amecheza mechi 6 za mtoano goli 0, Messi mechi 8 goli 0.

Mabao 10 ambayo yamefungwa katika mechi za hii leo yanaifanya siku ya leo kuwa siku ya pili ambayo kulifungwa mabao mengi katika hatua ya mtoano kombe la dunia baada ya siku ya tarehe 17 June 1970 ambapo kulifungwa mabao 21 katika nusu fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here