Home World Cup RUS 2018: utabiri wa Billnass, Kapombe, Ben Pol na mastaa wengine kuhusu...

RUS 2018: utabiri wa Billnass, Kapombe, Ben Pol na mastaa wengine kuhusu 16 bora! wazee wa kubeti mpo!!

11274
0
SHARE

Hatua ya 16 bora hiyo hapo. Kila mtu kwa sasa tumbo joto. Sio Ronaldo Sio Messi wala Kane wote wameshapewa somo na Korea Kusini kwamba ukubwa wa timu yako sio hoja. Hapa nakuletea uchambuzi na utabiri wa kila mchezo wa hatua ya 16 bora.

JUMAMOSI 30-06-218.

France vs Argentina. Saa 11:00 jioni.

Billnass
Mimi nashabiki Ufaransa. Unatarajia nitakupa jibu gani? Sawa Messi ni mzuri lakini amezungukwa na watu wasiojali bendera za taifa lao. Kwaheri Messi.

Ben Pol
Kaka Messi ni mtu mbaya sana lakini wafaransa wengi wanajituma. Sion mlango anaoweza kuipitia Messi. We mwenyewe si umeona walivyobebwa bebwa kwenye mechi yao na Nigeria. Messi hapo hapumui kaka, hiyo imeisha hivyo.

Enock Bwigane
Juzi nimesikia kauli ya Marcos Rojo akimsifia Lionel Messi kwamba ni kiongozi bora. Watu wengi wamezoea kuona kiongozi bora ni yule ambaye anapiga makelele uwanjani. Rojo anasema Messi alitupa mawaidha mazuri sana wakati wa kubadilisha mavazi. Messi miaka yote amekuwa akituhimiza namna ya kupambana”. Hivyo kwa mtazamo wangu sioni kama Samwel Umtiti atamzuia Messi. Hata huyo Varane sioni namna atakavyomzuia Messi. Nawapa nafasi kubwa Argentine.

Shomary Kapombe
Hawa Argentina tia maji tia maji tu. Wamepita kwa bahati sioni kama wanaweza kufanya chochote. Wana wachezanu wa kiwango cha juu kabisa lakini wameonesha kiwango kibovu sana

Uruguay vs Portugal. Saa 3:00 usiku.

Shomary Kapombe
Siwapi ushindi Uruguay kwa sababu ukiangalia mechi zao wamepata matokeo kwa tabu. Yaani hawapati matokeo yanayoendana na Ubora wa timu yao wanasuasua tu.

Bwigane
Ureno anapita vizuri tu. Uruguay wanasuasua sana. Wana timu nzuri lakini wanacheza kama timu ndogo. Waliweza kuzuilikana Misri vizuri tu sasa watatoka vipi kwa Ronaldo?

Billnass
Ureno ni timu inamtegemea mchezaji mmoja. Siwaamini hata kidogo hawa ndio mwisho wa safari yao.

Shaffih Dauda
Ronaldo hawezi kumuacha mtu salama hapo natoa nafasi kubwa kwa Ureno.

Ben Pol
Ronaldo ni mchezaji anayeweza kucheza timu yoyote tena kwa ufanisi ule ule. Huyo ndiye mwiba wa kwa Uruguay. Ureno anapita

JUMAPILI 01-07-2018.

Spain vs Russia. Saa 11:00 jioni.

Bwigane
Safari ya Warusi imeshia hapo Shekh. Hwa warusi kama sisi tu. Watumia zaidi nguvu kuliko akili. Wamefanya vizuri sawa lakini Shekh hadi Saudia unadhani hata sisi si tunawapiga!!!!

Billnas
Hata wewe hapo unajua kwamba Urusi wanapaswa kuwa mashabiki tu na si vinginevyo. Safari yao imeisha.

Shaffih Dauda
Hiyo mechi ni rahisi sana wala usitegemee miujiza. Hii ndio mechi itakayozalisha mabao mengi zaidi.

Kapombe
Napenda kuwashukuru Urusi kwa mapokezi yao lakini hatuna nafasi yao zaidi ya hapa walipofika.

Ben Pol
watu wengi wanaweza wasiipe nafasi Urusi lakini nataka niwakumbushe kwamba kucheza nyumbani kuna faida kubwa sana..

Croatia vs Denmark. Saa 3:00 usiku.

Bwigane
Moja ya timu ambazo zinacheza nafasi ya kiungo kwa kujiamini na weledi mkubwa. Mordic na Ivan wamefanya makubwa sana. Nawapa nafasi. Watu wengi wanaweza upande wa Denmark kisa yule kijana wa Tanga lakini sioni kama Ericksen na wenzake wanachakuwavimbia Croatia.

Shaffih Dauda
Kama Argentine waliwashindwa hawa Denmark wana kipi cha ziada cha kutuamanisha kuwa watawazuia?

Kapombe
Croatia wana wachezaji wengi wa kawaida lakini wanaojua nini maana ya timu ya taifa. Watashangaza wengi sana mwaka huu

JUMATATU 02-07-2018

Brazil vs Mexico. Saa 11:00 jioni.

Bwigane
Ni mechi ya upande mmoja. Siwapi nafasi kabisa Mexico.

Shaffih Dauda
Brazil anapita. Neymar akitulia vyema, Titte akatuliza kichwa bila shaka hakuna beki wa kuwazuia hawa viumbe. Brazil wana uwezo wa kucheza mpira wa iana yoyote ule. Kuna wakati watarilaxi uwanjani kuna wakayi watafanya msako, What a team! Nafasi kubwa nawapa wao

Billnas
kwakweli hiyo mechi usibet ndugu yangu. Shida ya Brazil hawaeleweki. Kesho wapo hivi kesho wapo vile. Usijitoe akili kuibeti achana nayo

Ben Pol
Brazil sio wazuri sana kama zamani. Lakini siamini sana kama Chicharito anaweza kurudia kile alichofanya uwanjani. Chicharito baada ya mchezo wa Ujerumani alilia, Neymar baada ya mechi na Costa Rica pia alililia. Watoto wa mama wote wanakutana. Nawapa nafasi kubwa Brazil

Kapombe
Mechi ngumu sana. Yoyote anaweza kuzishanda. Hapo 50 kwa 50

Belgium vs Japan. Saa 3:00 usiku.

Bwigane
Napata hofu kidogo kwa kwa Japan hasa kwa aina yao ya uchezaji. Wanacheza sana kitimu lakini bado itakuwa mechi ya upande mmoja. Nawapa nafasi kubwa Ubelgiji ingawa wasiwasi ni aina ya ukabaji wa Japan ambao unaweza kupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penati.

Shaffih Dauda
Sioni namna Japan atapita. Ubelgiji watapita kwa kishindo. Ubelgiji wana wanachezaji wanaojielewa sana. Wamepata mecho rahisi sana. Mchezo ungekuwa mgumu sana kama wangecheza na Senegal. Ubelgiji wana uzoefu mkubwa sana wala sitegemei maajabu katika mchezo huu.

Billnass
Kaka nani asiyewajua Ubelgiji bhana! Hebh niulize swal lingine kaka! Hao Japan watapita vipi sasa?

JUMANNE 03-07-2018.

Sweden vs Switzerland. Saa 11:00 jioni.

Bwigane
Licha ya kwamba Shaqiri na Xhaka watakuwepo lakini bado Sweden wanacheza mpira wa kujituma sana. Wachezaji wake wana nguvu, wana kasi na wanapambana. Kitendo cha kuwatoa Italia kwenye hatua ya mtoano basi ni dhahiri kwamba Uswisi watapata tabu sana

Shaffih Dauda
mhhhh mechi ngumu sana hii. Hii mechi kwangu kuitabiri. Ingawa Xhaka ni mtu mbaya sana. Bado nawaza sana namna huu mchezo utaisha.

Colombia vs England. Saa 3:00 usiku.

Bwigane
Inanikumbusha mwaka 1998 walicheza hawa jamaa. England wakiwa na kikosi chao bora kabisa akina Beckham na N.k. England ile ilifanikiwa kuifunga Colombia ikiwa na watu wenye uwezo wao na sio hii ya Sasa ambayo katika safu yao ya mshambuliaji wao bora Harry Kane hana hata mwenye medali ya kombe la kuku. Safu yao ya ushambuliaji ina vijana wachanga sana. Safari ya England imeishia hapo siwapi nafasi kabisa. Unapomwangalia Cuadrado tayati amecheza mechi mbili za Uefa za fainali, Falcao amecheza fainali tatu za Yuropa hivyo wana uzoefu mkubwa wa mechi ngumu. Colombia wana uwezo mkubwa wa kutafuta matokeo mpaka dakika za mwisho.

Shaffih Dauda
Harry Kane sio mtu mzuri. Ronaldo anapaswa kuwa makini sana la sivyo kiatu hapati. Mchezo ni mgumu sawa lakini Colombia weupe tu. Sioni niwatete kwenye engo gani lakini England wanatisha. Ni kweli Timu za Amerika zina uwezo mkubwa wa upambanaji mpaka dakika ya mwisho lakini England wana damu changa yenye uchu wa mafanimio. Yule Falcao wanamjua tokea akiwa EPL hawezi kuwasumbua hata kidogo.

Mtazamo wangu? Brazil, Uruguay, Spain, Denmark, Uswis, Argentine, Ubelgiji na Colombia

Credit kwa wote waliokubali kufanya mahojiano na mimi ni Privaldinho usiache pia kunifuatilia Instagram.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here