Home World Cup RUS 2018: Soka la Afrika lina dhahabu lakini tunaitumia kama kokoto

RUS 2018: Soka la Afrika lina dhahabu lakini tunaitumia kama kokoto

10736
0
SHARE

Mgema akisifiwa sana tembo hutia maji. Sawa Senegal walicheza vizuri, wakatubeba kimasomaso. Leo wamekwenda uwanjani na matokeo yao mfukoni. Wamecheza kama Yanga. Hawaeleweki wanaenda mbele au wanarudi nyuma. Leo Senegal wanapinduliwa na Japan? Shida ilikuwa wapi? Binafsi naona tu yale yale ya kujiandalia matokeo mkekani badala ya kwenda kutafuta matokeo uwanjani.

Sijui kwanini Cisse ametuacha mdomo wazi kiasi hiki. Juzi tulimsifia sana. Leo amecheza na Wauza unga waliokuwa hawajielewi. Kwani nani hakuona utumbo wa Colombia leo? Tunapaswa kujifunza kitu kupitia haya mapungufu. Daah nazidi kuamini kwamba asili ya mwafrika ni ngozi yake. Hawezi kuisaliti kamwe. Hivi unaikumbuka Mechi ya Kagera Sugar na simba pale taifa! Yaani unakwenda kukamilisha ratiba kwa kucheza kama hutaki? ilhali unajua unahistoria inakusubiria uikamilishe? Nimejiuliza Senegal walikuwa wanaenda kukamilisha ratiba ya nani?

Baada ya hapo naomba nitoe dukuduku

Je kuna sababu ya kumlaumu Cisse? Binafsi ndio. Sawa wametolewa kwa kadi 6 za njano dhidi ya 4 za Japan lakini kwanini wameenda kucheza kama wamekwisha kubeba ubingwa?

Unataka tuamini kwamba Senegal walizidiwa na Colombia? Tutakuwa waongo. Kilichotokea Senegal walifanya kupoteza muda uwanjani wakitegemea kitambaa kile kitawatosha sare.

Nimemsikia Mtangazaji wa huko uzunguni akisema “Sorry for Afrika but that should not be interpreted as the end of World Cup for them”. Anamaanisha Poleni Afrika lakini huu sio mwisho wa kombe la dunia! Ningekuwa karibu ningemwambia ikitokea sisi tumebeba kombe la dunia basi ujue hilo ni kombe la Afrika tumelibadilisha jina tukaamua kuliita hivyo lakini sio kile kinyago cha Gazzaniga.

Juzi nilijikaza kweli kuitetea Afrika nikiamini kuwa Senegal na Nigeria zitamaliza shughuli. Tuwapuuze waarabu wanaojua mpira lakini wanacheza kwa kiburi uwanjani. Poland kafanya kuisaidia kabisa Senegal. Poland kashajitokea lakini kambutua Japan. Senegal Kashindwa hata kupata suluhu? Kwa vurugu hili wangeenda kuwaambia nini England au Belgium

Kosa lingine kubwa nililoliona kwa Afrika ni Ukabaji wa macho. Yaani tunafungwa mabao ya mipira ya adhabu/iliyokufa kama kona na pigo dogo la adhabu. Beki aliyekuwa ana mkaba Yeri Mina yaani ni kama alikuwa anataka kumuomba jamaa namba za Messi kwa sababu tu yupo Barcelona. Wala hakujishughulisha kuangalia mpira unatokea wapi? una urefu gani, umekuja kwa kasi gan? yeye kaishia kumng’ang’ania. Achilia mbali huyo kuna mmoja alisisima kwemye nguzo kama sanamu, nikjiuliza tupo Vatcan au vipi maana kule Vatcan ndipo kuna sanamu nyingi za wakatoliki.

Kisha nimewaza sana. Unajua wachezaji wengi wa Afrika waliopo ulaya wana vipaji vikubwa sana kuzidi hata hale wa ulaya kama akina Hazard n.k. Unajua mpaka mchezaji wa kiafrika anafika ulaya amehaso mno. Yaani ni juhudi zake za kipaji cha kuzaliwa. Ukiona mtoto wa kata anafanikiwa ana pata Daraja la kwanza muogope sana. Narudia ukiona mtoto wa shule ya kata anapata daraja la kwanza au hata la pili muheshimu sana.

Messi akiwa na miaka 9 alicheza michezo ya ushindani hadi na timu nje ya taifa lao. Neymar akiwa na miaka 14 alifanya majaribio Real Madrid. Kylian Mbappe akiwa na miaka 12 amefundishwa na makocha wakubwa. Utamu wa chakula ni maandalizi mazuri jikoni. Sisi tunavyakula vizuri lakini tunavipika kwa kulipua.

UEFA na ligi mbalimbali huwa wanakuwa na vikao vya maendeleo ya soka ya maeneo yao. Wanakuwepo makocha wastaafu, makocha wale wazoefu na wale wanaochipukia. Lengo ni kugawana ujuzi. Wenzetu kila baada ya Kombe la dunia makocha wote wakubwa wakubwa huitwa. Hujadiliana kwanini timu fulani zilifanya vibaya.

Wanachambua kila mechi kisha wanatoa mawazo yao na wanaanda CD kwa ajili ya kujifunzia. Sisi kombe likiisha na habari inashia hapo hapo, sio CAF sio washiriki wote wanaingia mtini.

Nimejiuliza CAF hivi vikao vipi? Jata kama vinafanyika Je vina tija? Je shirikisho la soka Tanzania limepeleka makocha wangapi kujishikilia kweye vilabu vikubwa au mataifa ya ulaya? au hatujui umihumu wa akina Julio kama tutawaendeleza?. Ukikaa meza ya wakubwa hufi njaa utakula hata makombo. Tunakimbilia makocha wazungu ambao huwa tunawalazimisha kukusanya wachezaji wanaocheza ulaya au wale wanaocheza vilabu pendwa kwenye mataifa yetu kisha tunamwambia nenda nao kombe la dunia.

Shida kubwa Afrika sio wachezaji ila mifumo ya ufundishaji. Wachezaji wetu ni wazuri sana wanapokuwa ulaya. Afya nzuri haiji hivi hivi unapaswa ule vyakula vizuri. Mtu anakwambia ooh Mane boya tu, hajitumi kama Liverrpool. Akiwa Ulaya anakula Madini ya akina Klopp leo mnamleta Afrika mnampa kokoto? Sahauni!

Tumeelewana lakini! Tupeleke waalimu wetu ulaya wapate leseni kubwa kubwa waje huku watupe madini. Leo hii Tanzania hakuna kocha wa kumpa madini Samatta. Samatta anakuja tu kwa sababu ya utaifa. Hata sauzi hapo tu wanatuzidi makocha wanaguzid ufundi. Mwangalieni Banda wa Baroka na yule Banda aliyeenda Algeria na Taifa Stars

Naitwa Privaldinho nipo Instagram pia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here