Home World Cup RUS 2018: “Kombe la dunia limehatarisha uhai wa Mama”

RUS 2018: “Kombe la dunia limehatarisha uhai wa Mama”

9721
0
SHARE

Iran imepoteza mshambuliaji wake hatari sana ajulikane kama Sardar Azmoun. Ameachana na soka la timu yake ya taifa akiwa na miaka 23.

Wakati nasoma taarifa ya huyu jamaa nimekumbuka maisha yangu ya zamani wakati nakua. Nilikuwa napenda sana mpira. Licha ya kuwa na umbo dogo uwanjani lakini nilipewa jina la Privaldinho. Tatizo likaanza kwa bibi. Bibi alikuwa hataki kabisa kusikia mpira. Nakumbuka niliwahi kuvunjika mkono uwanjani bibi aliongea sana. Mwisho wa siku nikihamishwa hadi shule ili nisicheze mpira.

Ni kweli soka la bongo halilipi na kwenda ulaya sio rahisi. Kila mtaa nilioenda nilijulikana kwa sababu ya mpira. Nakumbuka kipindi naishi mwika majirani walinichukia kwa sababu tu nilikuwa nawahamasisha watoto wao kwao hawafanyi kazi ili tu tukacheze mpira. Malalamiko yote alipewa mama mkubwa aliyekuwa akiishi na mimi.

Huenda leo hii ningeitwa Messi wa Rombo/ Arusha.

Azmoun alipachikwa jina la ‘ Messi wa Iran’ kwa kutupia mabao 23 kwenye michezo 33 kwa timu yake ya taifa. Nadhani enzi zangu hata mabao 500 nilifikisha.

Iran chini ya kocha Carlos Queiroz walimiza watatu katika kundi B nyuma yaSpain na Portugal. Mchezo wao dhidi ya Ureno ulikuwa mchezo ulionivutia zaidi katika michezo yote ya hatua ya makundi na ule wa Mexico na Ujerumani.

Azmoun amesema kuchezea timu ya taifa ni maumivu. Amesema yeye kucheza timu ya taifa kunaweza kukampa jambo la kujivunia lakini familia yake ipo hatarini zaidi. Alifunga mabao 11 katika michezo 14 katika michuano ya kufuzu. Tatizo kubwa ni pale alipocheza kwa dakika 90 katika michezo yote mitatu ya makundi lakini akashindwa kufunga bao lolote.

Mashabiki wamekuwa wakimtumia meseji mbaya na matusi mengi kwenye mitandao ya kijamii wakidai kuwa alikuwa hajitumi hata kidogo. Amelaumiwa mno kwa timu yake kufeli sababu kubwa ni yeye. Iran ilifanikiwa kuifunga Morocco, wakapoteza kwa Spain and na kutoka sare dhidi ya Portugal.

Kwangu mimi sijaona sababu kubwa ya kuilaumu Iran hasa kuwepo katika kundi gumu kama hili tena wakiruhusu mabao mawili tu. Ujerumani na uzuri wao wote wameruhusu mabao manne katika kundi ambalo ambalo yupo Korea Mexico na Sweden.

Azmoun amesema mama yake ana presha kubwa sana. Watu wamekuwa wakipata mitaani wakimtukana yeye pamoja na familia yake. Mama yake anaposikia matusi hayo presha inapanda.

“Mama yangu kwa sasa anaumwa sana. Yote ni kwa sababu ya matusi na kejeli zinazosambaa mitandaoni. Siwezi kuendelea kujivunia kitu ambacho kinahatarisha maisha ya mama yangu,” Azmoun, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Russia ya Rubin Kazan.

“kuna watu wanakosa uvumilivu na ukarimu. Wamekuwa wanatutukana kwa jambo ambalo hatustahili. Hili suala limeniweka mimi katika mazingira magumu sana. Nipo tayati kumchagua mama yangu na kuachana na soka la kimataifa. Acha waite wachezaji ambao wao wanawaona watatimiza haja ya mioyo yao.”

Azmoun alianza kuichezea Iran akiwa na umri wa miaka 19 tu.

Akiwa na mika 23 tu tayati yeye ni mfungaji bora namba 5 katika taifa lao akiwa anafananishwa sana na nguli Ali Daei, mwenye mabao 109 katika michezo 149. Nguli huyo ndiye anayewatoa kijasho Messi na Ronaldo kufikia rekodi yake ya mabao mengi katika mechi za kimataifa.

Azmoun ni nani?
Ni mzaliwa wa jamii ya Sunni. Ana asili ya Uturuki na Irani. Baba yake alikuwa kocha mkubwa wa mpira wa pete. Anajua kwa ufasaha kituruki na Kiirani. Anavaa jezi namba 69 ambayo ni namba ya usajili ya magari katika mtaa aliozaliwa.

Alianza maisha ya soka akiwa na miaka 9 katika klabu ya Oghab Gongbad. Hakuwahi kucheza sana katika ligi ya Iran kwani alitimkia ligi kuu Urusi kwenye klabu ya Rubin Kazan. Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika ligi ya Urusi kutokea taifa la Iran. Wakati Azmoun anakwenda Urusi alikuwa na miaka 17 wakati huo mimi nishaachana na kucheza soka nikawa mwamuzi kwenye kombe la mbuzi shule ya Sekondari Malangali Iringa.

Alicheza mchezo wa kwanza akiwa na Rubin katika mechi ya Kufuzu UEFA. Mchezo wake wa pili waliceza dhidi ya Molde ambapo ilikuwa mchezo wa Europa league ambapo nngia dakika ya 64 na alifanikiwa kufunga bao. Mchezo wake wa kwanza wa ligi alicheza na Anzh Makachkala ambapo aliingia dakika ya 74 akafunga bao moja na kutengeneza lingine. Mchezo uliofuta aliwachapa Rostov bao moja, kisha mchezo uliofuta tena akawatungua Zenit bao moja.

Mzee Wenger si akamuona.. Daah Huyu mzee akaweka dau la Euro milion 2 Warusi wakakataa ofa. Barcelona, Ac Milan na Liverpool pia zikaweka nia Wenger akatoa dau lake. Baadae 2015 alipelekwa Rostov kwa mkopo. Rostov ilikuwa mbioni kushuka daraja. Mchezo wa mwisho wa Rostov kupambana kutokushuka daraja akatokea benchi na kwenda kufunga bao lililoiokoa Rostov kushuka daraja.

Baadae aliisaidia Rostov kumaliza nafasi ya pili mwaka 2016 kutoka kupigania kutokushuka daraja. Wakafanikiwa kwenda UEFA . Mchezo wake wa kwanza UEFA alikutana na Anderlecht ambapo alifunga bao lake la kwanza UEFA na kuisaidia timu kufuzu hatua iliyofuata. Kisha wakakutana tena na Ajax ambapo mchezo wake wa pili pia aliwatungua Ajax na kufuzu hatua ya makundi.

Bao lake la tatu UEFA aliwafunga Atletico Madrid licha ya kupoteza mchezo huo. Aliweka rekodi ya mchezaji wa kwanza wa Iran kufunga bao katika hatua ya makundi ya UEFA tokea Al Karimi mwaka 2005. Kisha alifunga bao lake la 4 baada ya kuwafumua bao moja Bayern Munich ambapo walishinda mabao 3 mawili na kuweka rekodi kwa Rostov kuwa ushindi wao wa kwanza katika hatua ya makundi.

Naitwa Privaldinho, usisahau kunifollow Instagram kwa jina hilo hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here