Home Kimataifa Shaffih Dauda aitoa Senegal World Cup, Nikki wa Pili haamini

Shaffih Dauda aitoa Senegal World Cup, Nikki wa Pili haamini

9501
0
SHARE

Kati ya matukio ambayo yaliwaumiza roho Waafrika katika michuano hii ya kombe la dunia baaasi ni matokeo ya Nigeria vs Argentina baada ya kushuhudia Nigeria akiyaaga mashindano ya kombe la dunia.

Lakini hii leo kuna mchezo mwingine kati ya wawakirishi pekee waliobaki wa Afrika timu ya taifa ya Senegal ambao watakaokipiga na Colombia katika kumtafuta anayekwenda hatua ya 16 bora.

Mchambuzi mkongwe wa soka nchini Shaffih Dauda yuko nchini Urusi na hii leo alikuwa na mahojiano na msanii wa Bongo Flava Nikki wa Pili na moja ya suala walilizungumzia ni nafasi ya Senegal hii leo.

Dauda anaamini hakuna nafasi ya Senegal hii leo kumfunga Colombia, Dauda anaamini linapokuja suala la mchezo kama leo ambalo timu ndio inatakiwa kufanya maamuzi na kuwa na concetration katika mechi ni ngumu kwa Senegal kushindana na Colombia.

Uwepo wa nyota kama James Rodriguez, Radamel Falcao, Cuadrado,Yerri Mina na wachezaji wengine wakubwa inawafanya Colombia kuwa na advantage ya wachezaji ambao wanaweza kuamua mechi wakati wowote tofauti na Senegal.

Shaffih amesema wachezaji wengi wa Afrika wanakuwa wanapoteza focus kadri muda unavyokwenda katika mashindano, na concetration yao katika nyakati muhimu inapungua tofauti na nyota wakubwa wa Ulaya na America.

Pamoja na maoni hayo ya Shaffih Dauda lakini rekodi za Senegal mbele ya timu za kutoka America sio mbaya sana, mara ya mwisho Senegal walikutana na Colombia 2014, Colombia wakaenda hadi half time wakiongoza 2-0 lakini mchezo kuisha kwa sare ya 2-2.

Mara ya mwisho kwa Senegal kukutana na timu kutoka America katika kombe la dunia ilikuwa 2002 dhidi ya Uruguay ambapo Senegal waliongoza kwa bao 3-0 lakini mchezo ukaisha kwa sare ya 3-3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here