Home World Cup RUS 2018: Pesa watakazopata Kane na Lukaku ni kufuru

RUS 2018: Pesa watakazopata Kane na Lukaku ni kufuru

16200
0
SHARE

Kama England watashinda World Cup mshambuliaji wao Harry Kane atapatahela nyingi zaidi ya kitita anachotarajia kusaini Spurs kwa wiki.

Matt Law anasema kuwa England wanakutana leo na maswahiba wao wa zamani Ubelgiji ambao walisaidiana wakati wa vita vya dunia kupingana na Dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler.

Matt Law amesema shirikisho la soka Uingereza limegoma kabisa kutaja kiasi watakachopokea wachezaji wao ikiwa watabeba ubingwa huo lakini mashilawadu wa England wamesema watabeba kitita cha £5 million ni sawa na Tsh 12,000,000,000 ambapo kila mchezaji atapeleka nyumbani £217,000 sawa na Tsh 650,800,000. Harry Kane, anatarajia kusaini mkataba mpya ambao utagharimu £200,000 sawa na Tsh 480,000,000, kwa wiki.

Ubelgiji ambao wamekuwa mashwahiba wa England kwa kipindi kirefu wao watapata £9.2 million sawa Tsh 21’600’000’000, kama bonasi yao na akina Lukaku wataondoka na £400,000 sawa Tsh 960,000,000 kiasi ambacho Radja Nainggolan atakisikia kwenye Tv mara baada ya kutemwa. Malkia wa England hivi majuzi mwaka 2007 aliitembelea Ubelgiji ambapo alipokelewa na Mflame Albert. England na Ubelgiji wanatawalia na familia za kifalme.

England imemuahidi kocha wao Gareth Southgate kwamba ataondoka na kitita £1.5 sawa na Tsh million. Mwaka 2006 Gareth alisemekana kununua jumba la thamani ya milion 3.5 Sawa na Tsh 3,600,000,000 lakini mapema mwaka 2017 aliliweka sokoni akitaka kuliuza baada ya kusema amekuwa akisumbuliwa na wageni na wezi. Nadhani pesa atakazopata baada ya ushindi wa kombe la dunia atanunua jumba lingine la kifahari zaidi atakalishi na mkewe Alison.

Kwa upande wa Ubelgiji watamzawadia kiasi cha £500,000 sawa na Tsh 1,200,000,000, kocha wao Roberto Martinez.

England watapokea kiasi cha £1 million (£43,478 sawa na Tsh 104,347,200 kwa kila mchezaji) kama bonasi ya kufika hatua ya 16 bora. Kama wasingefuzu wasingepata hata 10.

Ubelgiji wao wametenga £850,000 sawa na Tsh 2,044,800,000 kwa kitendo tu cha kwenda kombe la dunia. Yaani kuitwa tu timu ya taifa timu nzima imepewa kiasi hicho. Pia wametenga £1.61 million (£70,000 Tsh 168,000,000 kwa kila mchezaji) kwa kufuzu hatua ya 16 bora. Sijui akina kichuya na Samatta hawaoni huu mpunga.

Kama akina Neymar watafanikiwa kuipa Brazil Ubingwa kila mchezaji atakwenda kwao na £750,000 Tsh 1,800,000,000. Kama nawaona watakavyojaa Maraccana na kule Copa Cabana maana huo mpunga sio wa mchezo mchezo. Kikosi cha Ujerumani kimepoteza kitita cha £350,000 Tsh 840,000,000 baada ya kuondolewa na Korea Kusini.

Mwaka 1966 baada ya England kutwaa ubingwa wa dunia kila mchezaji alipewa kititia cha £1,000.

Mshindi wa kombe la dunia atakwenda kwao na £28 million Sawa na Tsh 67,200,000,000.

Yaani kama Tanzania mwaka 2022 tukishinda kombe la dunia basi akina Samatta watatuletea huu mpunga wa Maana. England na Belgium wamekwisha ahidi timu zao kupata £9 million kwa kitendo cha kufuzu tu hatua ya 16 bora.

Najiuliza sana mwaka 2022 Raisi Karia atatoa kiasi gani cha fedha kwa stars tukifuzu. Maana tupo vizuri, Huku Banda kule Samata, Pale Msuva kule Ulimwengu. Mbona watatukoma??

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here