Home World Cup RUS 2018: Chin Bees “VAR ni ya kinyamwezi”

RUS 2018: Chin Bees “VAR ni ya kinyamwezi”

12248
0
SHARE

Msanii wa muziki wa Hiphop anayejulikana kama Chin Bees amesema anaukubali sana mfumo wa VAR ambao umewatoa povu mashabiki walio wengi. Chin Bees nilikutana nae Escape one “kwenye soka la levya”. Fika Escape one ukutane na mastaa wakubwa unaowakubali wakifuatilia michuano ya kombe la dunia. Tukapiga stori moja mbili tatu. Nilipomuuliza taifa analoshabikia alisema kuwa anaikubali sana Brazil lakini haoni kama itafika mahali

“Nawakubali sana wanangu wa Brazil lakini wanatuzingua hawa. Hawajitumi kama waliowatangulia. Kama Brazil wangetulia hawa jamaa kwa namna walivyojaa vipaji wangekiwasha sana sema ubishoo mwingi utadhani wanabana pua”

Timu gani unayoamini itabeba kombe la dunia?

“Ubelgiji wakikaza ninaamini watabeba ndoo. Brazil miyeyusho. Belgium wapo vizuri. Huyo Lukaku hakamatiki. Ukikutana nao lazima uombe maji. Belgium nusu ya timu wote mastaa naa wanajielewa. Kikosi chao kina watu wanajioamini. Uwezo walio nao lazima wafanye kitu. Wapo vizuri sana wasipochukua kombe wajilauamu. Beligum watamu sana hata wakikutana na Brazil mimi nitakuwa upande wa Belgium. Pia namwelewa sana Batshuay anaonekana mshikaji sana, si unaona zile rasi diazini kama najiona Borussia”

Mchezaji gani unaamini atafanya vyema kombe la dunia?

“Kombe la dunia limekuwa gumu sana. Hupati hata muda wa kutema mate. Bado bingwa hajatabirika. Mambo yamekuwa magu sana hasa hasa kwa wale vigogo tuliowapa nafasi ye kubeba. Unaweza kusema hivi lakini mambo yakaenda mrama, kwa mfano hata mimi niliwaamini Brazil lakini nishaghairi”

Messi na Ronaldo yupi atatoka mapema kombe la dunia?

“Mimi namkubali sana Messi lakini daah, huyu Ronaldo timu yake inafanya vizuri zaidi. Wanajituma sana aisee. Ni tofuati na hawa wanaomzunguka Messi. Shida ya Argentina wanasuasusa. Hawafiki mahali popote hawa wanayumba sana. Ile siku Argentina amepita nilifurahi kiasi kwamba Lord Eyez akaniuliza mbona sio mzalendo wa Afrika. Namkubali sana Messi, amekaa kibababaye”

Timu za Afrika ulikuwa unaikubali timu gani?

“Nilikuwa nawakubali sana Senegal. Wale Senegel ni watu sema tu bahati yao mbaya. Kama wangefanikiwa kuvuka hii nafasi wangesumbua sana”

Unadhani kwanini Wajerumani wametoka mapema?

“Kwanza nimefurahi wametoka. Waliipiga timu yangu ya Brazil 7. Siwakubali wala hata siwaelewagi hata kidogo. Yaani nisumumunye maneno siwapendi hata kidogo. Siku wamefungwa niliruka sana. Wale tushawazoea kwa namna wanavyocheza. Mfumo wao ule ule, mwalimu yule yule hawakuwa na jipya. Timu ukishaigundua ni rahisi sana mipango yake kutibuliwa. Walikuja kimazoea. Walishambuliaji bila kujihami”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here