Home Kimataifa Nikki wa Pili na Shaffih Dauda na mitazamo tofauti England vs Belgium

Nikki wa Pili na Shaffih Dauda na mitazamo tofauti England vs Belgium

8598
0
SHARE

Pambano linalovuta hisia za watazamaji wengi hii leo ni Uingereza dhidi ya Ubelgiji, pamoja na wote wawili kuwa tayari na nafasi kucheza 16 bora lakini mshindi wa mchezo huu atakuwa anakwenda kama kinara wa kundi.

Katika michezo miwili kati ya timu hizi kwenye kombe la dunia Waingereza hawajawahi kupoteza, walipata suluhu ya bao 4-4 mwaka 1954 na wakashinda kwa bao 1-0 mwaka 1990 kwa shuti la David Platt dakika za nyongeza.

Lakini leo wanakutana tena huku Nikki Wa Pili akiamini kwamba Wabelgiji wanakwenda kuvunja mwiko wa kutoifunga Uingereza na kwa mara ya kwanza wanaenda kuwapiga katika kombe la dunia.

Nikki anaaamini Uingereza japo ina vijana wengi lakini wanaonekana wakomavu, akitolea mfano Harry Kane, Delle Ali, Jesse Lingard na Sterling. Pamoja na wachezaji hao lakini Nikki anaona utulivu wa Ubelgiji unaweza kuwaumiza Waingereza hii leo na kama Ubelgiji wakatangulia kwa goli hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa Uingereza.

Kwa upande wa Shaffih yeye anaona Uingereza na Ubelgiji leo ndio kama siku yao ya ufunguzi wa World Cup kwani timu ambazo hadi sasa wameshacheza nazo (Tunisia na Panama) zilikuwa ni timu nyepesi sana.

Kwa taarifa tu ni kwamba Ubelgiji wameshinda mabao 3+ katila mechi zao mbili zilizopita za kombe la dunia, hakuna timu katika michuano hii imeshawahi kushinda mabao 3/3+ mara 3 mfululizo na kama Ubelgiji watafanya hivyo itakuwa timu ya kwanza.

Lakini pia kwa Waingereza wenyewe kama watashinda mchezo wa leo baasi itakuwa mara yao ya kwanza kushinda mechi 3 mfululizo katika kombe la dunia tangu wafanye hivyo mwaka 1982.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here