Home World Cup RUS2018: Je World Cup itatoa mchezaji bora wa Ballon d’Or, Kaseja amtosa...

RUS2018: Je World Cup itatoa mchezaji bora wa Ballon d’Or, Kaseja amtosa Messi,

8399
0
SHARE

Juzi nilikuwa kijiweni na washkaji. Jamaa mmoja akasema Ronaldo mwaka huu lazima abebe kiatu. Mwingine akasema hana jipya ni mfungaji bora tu wala sio mchezaji bora. Mabishano yalikuwa makubwa mwisho wa siku hakukuwa na maelewano. Mmoja akaniambia wewe si unachambuaga mpira tupe mtazamo wako. Niliwapa jibu moja tu. Ronaldo hakufurahishi kwa uchezaji wake lakini anakupa sababu ya wewe kujipiga kifua mtaani.

Lakini msimamo wangu bado ni ule ule kwamba kiwango cha Mo Salah msimu huu kimenikosha zaidi.

Takwimu za ronaldo zinabadilika sana. Tena mara kwa Mara. Miaka 33 anawafanya watu wamtazame kwa lugha tofauti.

Nilipata bahati ya kuongea na Juma kaseja. Juma Kaseja wakati naamuuliza kuhusu kombe la dunia kama linaweza kutwaa Bingwa wa Ballon d’Or alinijibu hivi.

Ukitaka kujua alichoongea Kaseja kama kombe la dunia litatoa mchezaji bora wa dunia

click hapa/Bonyeza hapa

Miaka kadhaa ya nyuma kombe la dunia lilitoa wachezaji bora wa dunia. Kwa mfano mwaka 2006 Fabio Canavaro alibeba tuzo kwa mafanikio ya taifa lake kutwaa ubingwa wa dunia.

Mwaka 2002 Ronaldo De lima akiliongoza taifa la Brazil kule nchini korea alifanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia kwa kumtungua Oliver khan. Mwisho wa siku De lima alibeba ubingwa wa Ballon d’Or.

Mwaka 1994 Robberto Baggio alishindwa kubeba Ballon d’Or yake ya pili mfululizo licha ya kwamba taifa lake lilifika fainali ya kombe la dunia. Brazil waliifunga Italia kwenye fainali, Kwanini hakuna mchezaji wa brazil aliyeingia tatu bora? Kwa sababu Hristo Stochkvic aliibuka kinara wa kombe la dunia kwa mabao wala hakuna mchezaji wa Brazil aliuefanya vyema zaidi yake. Hristo alifunga mabao matano kwa Bulgaria kwenyr michuano ya kufuzu, kisha akafunga mabao 6 kombe la dunia na kutwaa kiatu cha dhahabu. Kubwa zaidi ni kuiondoa Ujerumani Magharibi waliokuwa mabingwa watetezi katika hatua ya Robo fainali.

Kumbe inawezekana usibebe kombe la dunia lakini ukafanya vyema na kutwaa tuzo hiyo. Hivyo Ronaldo hata kama Ureno haitofika fainali lakini wingi wake wa mabao ni kigezo tosha.

Lothar Matthaus alibeba Ballon d’Or baada ya kuchukua kombe la dunia mwaka 1990

Kwa ufupi tu. Inawezekana kubeba Ballon d’Or kupitia kombe la dunia lakini kuna mambo kadha wa ladha nimegundua. Kwanza lazima tuangalie mfungaji bora amefanikiwa kwa kiasi gani? Je kama umemebeba kombe la dunia je umefanya vizuri kuliko yule mfungaji bora. Kwa hiyo inawezekana kabisa mfungaji bora au mchezaji bora wa kombe la dunia akatwaa tuzo hiyo bora kabisa. Ingawa kwa siku za usoni wachezaji bora wa kombe la dunia wametoswa na Messi na Ronaldo.

Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here