Home World Cup RUS 2018: Brazil ni gari zuri lenye dereva asiyejiamini

RUS 2018: Brazil ni gari zuri lenye dereva asiyejiamini

9211
0
SHARE

Nilikuwa nimekaa na rafiki yangu mmoja nikamwambia Brazil ya sasa ni ngumu sana kusumbuliwa na timu za ulaya labda tu Ujerumani na Ufaransa. Nilinena haya kutokana na historia zao za hapo awali. Kauli yangu sio sheria lakini kwa uwezo walio nao Brazil kwa mchezani mmoja mmoja ni tishio hasa kwa mataifa yanayocheza soka la kufundishwa.

Takwimu zinaonesha kwamba ni timu 3 tu kutoka ulaya ambazo zimeifunga Brazil mara nyingi zaidi. Timu hizo ni Hungary, Norway pamoja na Uholanzi. Hakuna timu ambaye idadi walizoshinda ni nyingi zaidi ya Wabrazil hasa walipokutana.

Brazil wana wachezaji wenye ujuzi mkubwa na uwezo wa kukaa sana na mpira. Shida yao labda tuseme ni benchi lao la ufundi hasa kwenye mfumo wa uchezeshaji. Kumekuwa na kigugumizi cha namna gani kocha apandikize mbinu gani kupata ile krimu wachezaji waliyo nayo.

Mbali na ubora wao wa sasa Brazil wana rekodi kubwa sana ambayo inatembea kwenye damu za akina Coutinho na Thiago Silva. Kama ilivyo hela za wahindi kutembea kwenye damu za ukoo wao vivyo hivyo soka hutembea kwenye miguu na akili za Wabrazil. Maji hufuata mkondo. Mpaka sasa Brazil imecheza na mataifa 86 yanayotambulika na FIFA na imeshinda michezo 605 kati ya 956 na kupoteza michezo 197 pekee. Kizazi cha sasa kimeendeleza rekodi ya hapo awali, mara baada ya Silva kufunga bao la 226 ikiwa kuifanya Brazil iweke rekodi ya kufunga mabao mengi katika historia ya kombe la dunia.

Kuna watu wamekuwa wakilalamikia uwepo wa Paulinho kikosini.

Sawa, kwa kiasi fulani naweza kukubali kuwa ni mzito. Huhitaji darubini kuona hilo. Lakini Wachezaji wengi wa Brazil hasa safu ya ushambuliaji ni softi sana. Yaani wengi wao walaini mno.

Wananyumbulika, ndio,… wana vipaji, Sawa,…. wana kasi, hakika sina shaka,… Lakini hakuna hata mmoja wao anaweza kucheza jihadi (mabavu). Ili umpate mchezaji huyo itabidi usafiri mita takribani 30 mpaka 50 ndipo utakutana na Casemiro au Fernandinho dimba la kati. Umuhimu wa Paulinho ni nguvu na anaweza kuleta vurugu ambalo litawaweka bize mabeki na kuwapa uhuru akina Jesus.

Wala namba hazidanganyi.

Neymar na Jesus kwenye kikosi cha Titte ndio wenye mabao Mengi kumzidi Paulinho. Wote wana mabao 10, na Paulinho ana mabao 8. Umeona kazi ya Paulinho? Au bado hujaridhika? Umuhimu mwingine wa Paulinho umemfanya Coutinho awe huru na majukumu ya kukabia dimba la juu. Limemfanya awe mzururaji mwemye madhara makubwa zaidi kwa Brazil.

Coutinho hana haja ya kurudi chini kumsaidia sana Casemiro wala hana haja ya kukurupushana na mabeki. La Hasha hiyo ni kazi ya Paulinho. Kufikia sasa Coutinho amefunga mabao manne na kutengeneza mawili katika michezo 7 ya Brazil kwa mwaka 2018.

Inawezekana kipigo cha mabao 7 kwa Ujerumani kipo kwenye akili za wengi.

Sawa lakini kuna mabadiliko kidogo kiufanisi katika kikosi chao ambayo ni ngumu kuyakataa. Sio vyema kuwabagua sana eti kisa tu Neymar anajirusha. 2010 Brazil ilishinda michezo yake miwili ya mfululizo ya makundi. 2014 hawakuweza kufanya hivyo. Mwaka huu wameshinda michezo miwili mfululizo. Hii ni dalili nzuri kwao.
Bado wanzidi kulinda heshima za wahenga wao. Brazil wamefanikiwa kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya 13 mfululizo tokea miaka ya 1970.

Kuhusu mchezo wa na Serbia….. mhhhhhhh Tunaweza kusema wamekutana na vibonde katika mchezo wa leo. Serbia sio timu tishio sana. Hawana jipya katika kombe la dunia wametolewa kwenye hatua ya. makundi mara ya tatu sasa wakiwa kama taifa huru, 2006, 2010 na 2018.

Serbia wameanza kushiriki kombe la dunia kama taifa huru mwaka 2006. Nilishangaa sana wale waliokuwa kwenye TV wakisubiria kuona maajabu ya Korea kusini dhidi ya Ujerumani yatokee kwa Serbia pia. Pole sana kaka Masoud Issa CPA. inawezekana lakini Serbia wamefungwa michezo 7 kati ya 9 ya kombe la dunia. Sasa hii ni timu wa wasindikizaji? Kaka Issa kabla hujaomba lifti soma kwanza pleti namba usije ukajikuta unaomba lifti kwenye difenda ya FFU.

Kuna mtu mkubwa sana anaishabikia Ujerumani. Samahani sitomtaja jina. Nilipokutana nae Escape One wakati wa Ujerumani akicheza na Mexico nilishindwa kuonesha hisia zangu kwamba nipo upande upi baada ya kugundua kuwa yeye alikuwa upande tofauti na wa kwangu.

Wakati mwingine inabidi ufiche hisia ili kibarua kisiote nyasi. Enewei. Hii sio mara ya kwanza Ujerumani kufeli kule Urusi.

Mara ya kwanza Hitler alikwenda kichwa kichwa kwenye vita vya dunia vya Pili. Alichokosea alikwenda kipindi cha majira ya joto. Jeshi la Urusi likakimbia. Wakajifanya kama wameogopa vita. Wakati wajerumani walipokuwa wakihangaika kuua watu wasio na hatia vijijini majira ya baridi yaliikuwa mbion kuingia. Jeshi la Ujerumani likawa kwenye harakati za kutafuta zilipo kambi za Warusi. Mbaya zaidi muda ulizidi kwenda. Kufikia mwezi juni mwaka 1941 Hali ilikuwa mbaya kwa wajerumani kwani hawakuwahi kuzoea kuishi kwenye barafu. Jeshi la Urusi likaibuka upya. Wajerumani wakapata kipigo cha mbwa koko.

Kwa bahati mbaya tena leo Low ameenda kichwa kichwa. Anashambulia hovyo bila balansi nzuri ya kujilinda. Kauli chafu na majivuno kwa timu na wachezaji ni moja ya vichocheo vya mkosi wao. Mats alisema Leroy Sane asijione mchezaji mkubwa. Yeye bado mchanga sana wala hana msaada mkubwa kama Ozil na Muller. Nadhani Mats ametufundisha kuepukana na uropokaji.

Jog low mwenyewe alisema kuwa Sane amechelewa kufika mechi za kimataifa akimaanisha kuwa Sane haendani na falsafa zake. Walijiamini sana. Walijiona kama wanacheza wenyewe uwanjani. Hakuna nidhamu kubwa vitani kama kujihadhari na kumheshimu adui yako. Poleni sana wadau wa Ujeruman mimi timu yangu Irani.

Makala hio Imeandikwa na Privaldinho. Unaweza pia kunifollow Instagram

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here