Home Kimataifa Kombe la mabara ndio jinamizi lililowaumiza Wajerumani kombe la dunia

Kombe la mabara ndio jinamizi lililowaumiza Wajerumani kombe la dunia

12415
0
SHARE

July 2 mwaka jana timu ya taifa ya Ujerumani ilitwaa kombe la mabara pale nchini Urusi kwa bao pekee la Lars Stindi dakika ya 20 vs Chile, Wajerumani waliokua wakiongozwa na 80% ya timu B wakarudi nyumbani na ndoo mkononi lakini kumbe ilikuwa laana ya kueleka Urusi 2018.

Kabla ya Ujerumani kubeba ndoo ya mabara  kombe hili lilikuwa likiwatesa watangulizi wao wengi waliolibeba na yeyote aliyetwaa ndoo hii alionekana kupata matokeo hasi katika michuano iliyofuata ya kombe la dunia.

1992 Argentina. Mwaka 1992 wakiwa bila Diego Maradona Argentina walitwaa kombe la mabara pale Saudi Arabia, 1994 wakaenda Marekani katika kombe la dunia na wakaondolewa na Romania katika 16 bora huku nyota wao Diego Maradona akikosa mchezo huo kwa kile kilichotajwa kuwa matumizi ya madawa ya kusisimua mwili.

1997 Brazil. Mwaka 1997 ikawa zamu ya Wabrazil wakatwaa kwa kombe la mabara kwa kuipa kipigo cha mbwa koko Waaustralia cha mabao 6-0, 1998 Wabrazil wakaenda Ufaransa kwenye kombe la dunia wakionekana kuwa na matumaini ya kutwaa ndoo, lakini katika fainali ya michuano hiyo Wabrazil walishangazwa na wenyeji baada ya kipigo cha mabao 3-0.

1999 Mexico. Wakiwa kama wenyeji wa michuano hii mwaka 1999 Mexico waliibeba ndoo ya mabara kwa kuipiga Brazil katika mchezo wa fainali kwa penati 4-3, mwaka 2002  Wamexico wakaenda Japan na matumaini kibao lakini wakatolewa katika 16 bora na wapinzani wao wakuu timu ya taifa ya USA.

2003 Ufaransa & 2005 Brazil. 2003 katika fainali isiyofutika kichwani mwa Waafrika bao la Thiery Henry linawaua Cameroon katika fainali huku Marc Vivien Foe akifariki, miaka miwili baadae michuano hii inapigwa na Wabrazil wanaipiga Argentina 4-1, 2006 Brazil wanawaondolewa na Zizzou katika robo fainali lakini fainali Ufaransa wanapigwa na Italia huku Zidane akila kadi nyekundu.

2009 Brazil. Safari hii michuano hii ikapigwa Afrika huku Brazil na USA zikitinga fainali, mabao mawili ya Luis Fabiano na moja la Lucio likawaua Wamarekani na Brazil akaondoka na kombe, 2010 Felipe Melo anaigharimu Brazil katika robo fainali na wanaondolewa na Uholanzi huku Wahispania wakibeba kombe la dunia.

2013 Brazil. Michuano ya mabara inakwenda kupigwa Brazil huku wenyeji wakionekana hawashikiki, Paulinho aliwabeba katika nusu fainali kwa bao pekee dhidi ya Uruguay na wanakwenda fainali kukutana na Hispania, Brazil wanaichapa Hispania 3-0, 2014 kombe la dunia linapigwa nchini Brazil na wanadharilika kwa kipigo cha mbwa koko cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here