Home Kimataifa AC Milan wapigwa pingu kushiriki michuano ya UEFA

AC Milan wapigwa pingu kushiriki michuano ya UEFA

9964
0
SHARE

Klabu ya soka ya Ac Milan ya nchini Italia imejikuta matatizoni baada ya shirikisho la soka barani Ulaya Uefa kuwafungia kushiriki katika michuano yao.

Milan walikuwa wamefudhu kwa michuano ya Europa msimu ujao lakini sasa hawatashiriki michuano hiyo kutokana na adhabu hiyo iliyotokana na kukikuka sheria za matumizi Financial Fair Play.

Katika dirisha lililopita la usajili Ac Milan walitumia kiasi cha £200m kufanya usajili na UEFA wanaona kuna pesa ambayo imeingizwa nje ya mapato wanayopata Ac Milan.

Milan wenyewe kabla ya hukumu hii kutolewa walituma video katika mtandao wa Twitter wakisema wanataka haki na usawa ufanyike katika utoaji wa hukumu yao.

Bado Ac Milan hawajatoa taarifa yoyote baada ya hukumu hii lakini kama wakishindwa kukata rufaa baasi nafasi yao katika michuano ya Europa itakwenda kwa klabu ya Fiorentina.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here