Home Kimataifa RUS 2018: Messi anadaiwa na bibi yake.

RUS 2018: Messi anadaiwa na bibi yake.

10533
0
SHARE

Leo ndio leo tutajua hatma ya Leo Andreis Messi Cuccittin katika kombe la dunia. Juzi Messi alisheherekea siku yake ya kuzaliwa. Baada ya kukosa Penati mchezo wao wa kwanza siku ya jumapili Messi alijifungia ndani siku nzima. Juzi hatimaye furaha yake imeonekana tena. Ni mara baada ya uongozi wa timu na wachezaji kumfanyia Messi hafla fupi ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Messi amefanyiwa sherehe na bado anadaiwa bao na bibi Alicia Cuccititini. Alicia Cuccittin alikuwa mke wake Antonio Cuccittini ambaye ni babu yake na Messi. Babu yake Messi ndiye mtu aliyewajengea familia ya Messi nyumba ya kuishi. Bibie Alicia alikuwa akipenda sana soka. Siku ya kwanza kabisa Messi kwenda uwanjani ilikuwa Oktoba 1993 akiwa na Alicia. Bibi yake Alicia alikuwa akipenda sana mpira.

Messi anasema ” Bibi yangu alikuwa anakuja kutuangalia pale Rossario. Nilipokuwa Newells bibi aliniambia una kitu cha tofauti kushinda wachezaji wote kikosini kwetu. Alinisihi kuwa siku moja nitakuwa mchezaji mkubwa. Sasa nimefika mbali na hayupo nasi. Nimefika pale aliponitabiria lakini hayupo ila naamini kuwa bado ananiona”

Messi amekuwa akinyoosha vidole juu kwa ishara ya kumkubuka bibi Cuccittini. Bibi Cuccittin alifariki dunia mwaka 1998.

“Zamani mimi na Rodrigo (Kaka yake) Tulikuwa na ugomvi mkubwa sana. Ugomvi wetu ulikuwa kulala nyumbani kwa bibi. Tulikuwa tunampenda sana. Siku ya kwanza kwenda uwanjani alininunuliwa viatu vya mpira sitosahau. Alitupa kila kitu. alikuwa na moyo wa kipeke. Kila goli ninalofunga lazima nitazame juu kumkumbuka kwa fadhila zake”

Mzee Antonio Cuccittin alifariki dunia mwaka huu mwezi wa pili. Shida ni pale mzee Antonio aliponukuliwa akisema Messi bado ana deni kubwa kwa taifa lake.

“Messi ni mchezaji mkubwa. Siwezi kumtetea kwa kuwa tu ni mjukuu wangu lakini bado amefunikwa na kivuli cha Maradona. Tunahitaji atufanyie jambo la kukumbukwa lasivyo ataheshimika ugenini lakini sio ndani ya taifa letu.

Argentina watakutana na Nigeria. Argentina watahitaji kushinda zaidi ya bao moja halafu wao kutoruhusu bao lolote kisha kuwaombea Iceland wasuluhu au watoke kapa.

Argentina anadaiwa bao 2, Iceland anadaiwa bao moja na wote wana alama moja moja. Hivyo Argentina itahitaji zaidi ya mabao mawili zaidi ya yale watakayofunga Iceland.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here