Home World Cup RUS 2018: Afrika tumemkosea nini Maradona?

RUS 2018: Afrika tumemkosea nini Maradona?

9386
0
SHARE

Baada ya mchezo wa Argentine na Nigeria, nilikuwa narudi zangu nyumbani. Njiani nimekuta na jamaa mmoja anatukana sana. Anatukana ovyo oyvo, matusi yake yote aliyalekeza kwa Ighalo na VAR. Kwa kuwa sikumjua jina wala kufahamiana nae nikampoteza nisije nikapigwa vitasa.

Kuna rafiki yangu anaitwa beka, anampenda Messi kuliko anavyopenda kula. Nilipofika ndani kwangu jamaa akanigongea. Alipoingia ndani furaha aliyokuwa nayo ni zaidi ya kuongezewa mshahara. Alipiga magoti huku anasisitiza akaniambia kaka kesho ningeweka wapi uso wangu!

Huyu Beka kwanza ameningizia hasara ya glasi yangu amevunja kwa shangwe zake. Inaonekana leo hata watu weusi uzalendo waliuweka pembeni. Timu Messi kama nawaona vile na furaha yap. Sawa. Tuachane na hayo

Nilipowasha simu, kila kundi la whatsapp lina watu wanamtukana Maradona.

Wakati Argentine walipopata bao lao la pili kupitia Marcos Rojo Maradona ameonakana kushangilia kiasi cha kuchanganyikiwa na kuoneshaishara ya kidole kama tusi. Nimejiuliza sana. Ametutukana wafrika au kutokana na hali yake ya uhuni imekuwa mazoea kutukana kwake?

Ila Siamini sana kama amelenga ubaguzi au amewalenga timu Ronaldo ila Maradona ni mhuni tokea zamani. Historia yake ipo hivyo.

Inaonekana hasira za hasa hasa wale wa mrengo wa pili zimeleekea kwa Maradona. Wengi waliomba sare lakini kitambaa hakikutosha.

Maradona ni mmoja ya wahamashaji wakubwa kaatka timu yao ya taifa. Wengi wamekuwa wakimwekkea maneno mdomoni. Ametoka na kuweka hisia zake wazi kwa taifa lake. Ameweka pembeni umaarufu na ufalme wao na Messi. Hajajali sana ushindani wao ila uzalendo kwanza

Maradona ni mhuni. Nashangaa watu wakimwelekezea hasira zao. Watu nanatokwa aapovu kweli kweli. Mtu atatoka jasho kabisa kisa maradona ametukana. Ni kweli Maradona ametukana laakini hayo ndiyo maisha yake. Bata hana choo ndugu zangu. Najua maonbi yenu yalikuwa upande gani. Sawa amekosea sana. Mno. Amekosea haswa. Ni kweli naungana nanyi kuwa hafai kuigwa lakini uungani nanyi kwenye kutokwa povu. Lakini nisemme tu kama utahangaika na Maradona utapata tabu tu.

Hivi mmesahu kuwa aliwahi kususia sherehe za FIFA? FIFA walianzisha tuzo za mchezaji wa karne. Kura zilikuwa za wazi. Maradona akapigiwa kura kwa asimilia 53.60 Pele akapata 18. Muda ule ule kamati ya FIFA ikatengeneza tuzo nyingine ilimradi tu wampe Pele. Maradona alipokea tuzo yake akabeba zake akaondoka kabla Pele hajapewa. Akaacja ehehe inanendelea. Kimssingi sio jambo la kimichezo. Maradona akasema anajua waingereza wametengeneza tuzo za FIFA wakijua kuwa Pele anapendwa na kukubalika lakini wamefeli. Naona wametengeneza tuzo zingine za kinafiki. Ikumbukwe Maradona aliwafunga Waingereza bao la mkono. Kisha akawakejeli kwamba Mpira ulimgusa kichwa na mkono wa mungu ukagusa mpira kidooogo.

Mwaka 2002 Maradona alikumbwa na kesheshe za madawa ya kulevya na maisha yake kudorora. Mwandishi mmoja alimfuata ili kumhoji. Akampiga vibao yule mwandishi wa habari na kupasua kioo cha gari la mwandishi. Baadae alipohojiwa kuhusu kumpiga mwandishi yule alijibu akasema
“Mwaka 1986 nilitangaza bao langu dhidi ya England kuwa bao la mkono wa mungu, na natangaza rasmi kuwa kile kibao kilitokana na mkono wa sababu. Pia kuna siku alishuka kwenye gari na kumfuata mwandishi mmoja wa habari na kumpiga kibao kwa madai kwamba alimkonyeza Mpenzi wake zamani.

Miezi kadhaa kabla ya kombe la dunia mwaka 1994 Maradona alifyatua risasi angani ili kuwafukuza waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake.

Ikumbukwe pia miaka kumi nyuma yaani mwaka 1994 Maradona alipigana uwanjani na wachezaji wa Athletic Bilbao wakati yeye akiichezea Barcelona. Mchezo huo Barcelona walipoteza kwa bao 1. Baada ya mchezo Maradona alionekana kurukia watu mateke na vurugu kubwa kutokea.

Kombe la dunia mwaka 1994 Mashabiki wa ujerumani waliwazomea Argentina wakiimba wimbo wa taifa. Argentina ilikuwa inachukiwa sana na yote ni kwa. sababu ya tabia mbaya za Maradona. katika mchezo wa fainali kule jijini Rome katika uga wa Stadio Olimpico Argentina ilizomewa sana. Maradona alikwenda kwenye kamera na kutukana mara mbili. Alitumia kauli kama “hijos de puta” wala huhitaji kuwa Mspanyol au Mreno kujua maana ya maneno haya.

Maradona na uhuni wake na ujanja wake wote lakini Andreas Brehme aliyeokoa mikwaju ya penati ya Argentina mwaka 1990 alimfanya Diego alie kama mtoto mdogo huku akiwa na medali yake shingoni.

Wala msitegemee sana Maradona kuwa alama ya vidole aliyoonesha kwake ni shida sana. Anaweza akaomba radhi kinafiki tu lakini hatomaanisha. Na hatuna uhakika kuwa atabadilika lini. Juzi tu mchezo wa kwanza alionekana akivuta sigara uwanjan, Ni mhuni sana. Pele mwaka 2009 alisema kwamba “Diego is a bad role model” Alimaanisha kuwa Maradona hafai kuigwa. Huku akilenga zaidi kuwa anawathiri watoto hasa kwa tabia yake ya madawa ya kulevya.

Baadae Maradona aliamua kumjibu kwa kumtusi matusi ya nguoni akasema “sasa huyu namjibu nini? nani asiyejua kuwa aliwahi kuwa na mwanaume?”

Amekosea sana lakini ndivyo alivyo an atabaki kuwa hivyo labda aamue mwemyewe kubadilika hasa hasa ukiangalia umri wake umeenda.

Mwisho tukubali. Maradona ni mhuni. Sidhani kama amelenga kuwa sisi ni wafrika. Yeye kwa kuwa nimhuni na yale ndiyo maisha yake.

By Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here