Home Kimataifa Rekodi zilizowekwa J4 ya leo wakati Rojo akiwaliza Waafrika

Rekodi zilizowekwa J4 ya leo wakati Rojo akiwaliza Waafrika

8318
0
SHARE

Australia 0 – Peru 2, Paulo Guerrero aliyefunga bao la 2 la Peru ana umri wa miaka 34 na siku 176, anakuwa mchezaji wa 3 kutoka Amerika Kusini kufunga bao akiwa na umri mkubwa baada ya Martin Pelermo(miaka 36 na siku 227) na Jacinto Verela(miaka 36 na siku 279).

Bao la kwanza la Peru lililofungwa na Andre Carillo limewafanya Peru kuongoza katika mechi ya kombe la dunia tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwaka 1978 wakati wa mchezo kati ya Peru vs Iran.

Mara ya mwisho kwa timu ya taifa ya Peru kuwahi kushinda mchezo katika kombe la dunia ilikuwa mwaka 1978, tofauti ya kipindi hicho hadi leo ni miaka 40 na siku 15.

Dernmark 0 – France 0, mchezo kati ya Dernmark na Ufaransa ilikuwa ni mchezo wa 37 wa michuano ya kombe la dunia lakini huu ndio ulikuwa mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kuisha kwa sare ya 0-0.

Nigeria 1 – Argentina 2, kikosi cha leo cha Argentina kilikuwa na wastani wa umri wa miaka 30 na siku 189, hiki ndio kikosi chao chenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuanza katika kombe la dunia.

Mlinda lando wa Argentina hii leo alikuwa Franco Armani, huyu ni mlinda lango wa 17 kuwahi kuidakika Argentina katika kombe la dunia, hakuna nchi ambayo ina rekodi ya walinda mlango wengi kama Argentina.

Wakati mara ya mwisho kwa Messi kufunga katika kombe la dunia ilikuwa mwaka 2014 dhidi ya Nigeria na leo akafunga tena, Marco Rojo naye katika mabao 3 aliyowahi kufunga katika kombe la dunia, 2 yalikuwa dhidi ya Nigeria.

Iceland 1 – Croatia 2, Croatia sasa wanakuwa wametoa vipigo 3 katika timu zote walizokutana nazo katika kundi lao, hii ni mara ya kwanza katika historia ya Wacroatia kuwahi kushinda mechi 3 mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here