Home Kitaifa Huo mshahara wa Kagere Simba mmmh!!

Huo mshahara wa Kagere Simba mmmh!!

22541
0
SHARE

Tayari picha zimeshaenea kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mshambuliaji Meddie Kagere akisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Simba.

Kagere amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya. Ishu ni dau la usajili na mshahara wa jamaa, unaambiwa si mchezo.

Kwa taarifa ambazo si rasmi, inaelezwa saini ya Kagere imeigharimu Simba $50,000 zaidi ya Tsh. 110M huku mshahara atakaovuta kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili ukiwa ni $5,500 zaidi ya Tsh. 12M.

Meneja wa mchezaji huyo Patrick Gakumba ameiambia www.shaffihdauda.co.tz tayari Kagere ameshasaini mkataba Simba kilichobaki ni kutangazwa hadharani.

“Deal inakaribia kuisha kwa sababu tumesha kubaliana na kuafikiana, amesha saini kilichobaki ni Simba kumtangaza hadharani. Kila kitu kinaenda vizuri na tumeafikiana vizuri”- Patrick Gakumba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here