Home Kimataifa RUS 2018: Nani atafuzu au kushika nafasi ya 1/2 Kati ya Ureno...

RUS 2018: Nani atafuzu au kushika nafasi ya 1/2 Kati ya Ureno na Hispania?

9699
0
SHARE

Ronaldo anakutana na Iran. Iran sio tishio sana lakini kombe la dunia mwaka huu ndio tishio hasa. Ronaldo mabao manne kufika sasa. Mabao mengi kuliko kikosi chote cha Iran. Iran wana bao moja pekee.

Kombe la dunia la mwaka huu limekuwa na matokea ya ajabu sana. Timu ndogo zimefanya mambo ya ajabu mno. Ureno watakwenda katika mchuano huu wakijua kwamba sare yeyote au ushindi utawapeleka hatua ya mtoano.

Ureno ana ambao Manne ya kufunga na Matatu ya kufungwa. Jumla ana tofauti ya bao Moja. Iran ana bao kufunga na bao moja la kufungwa. Hispania yupo sawa na Ureno kila kitu.

Je itakuwaje kama Ureno atafungwa bao Moja au Ureno wakilingana kila kitu na Hispania yupi atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa pili au wa tatu. Wote watakuwa na tofauti ya bao Moja.

Sheria FIFA zinasemaje.

Endapo Timu zitalingana katika alama
1. Alama
2. Tofauti ya Magoli
3. Magoli ya kufunga

Kama watalingana katika mambo mawili au matatu, yafuatayo yatazingatiwa.

1. Alama zilizopatikana kwa timu zote zilipokutana.
Kwa mfano:
Kama Ureno akishinda 1, Hispania akashinda Moja. Maana yake watakuwa sawa kila kitu. Hii sheria hapa haina mashiko kwani mchezo wao wote waligawana alama. Hivyo yafuatayo yatazingatiwa
1.1. Kadi ya kwanza ya njano hupunguza alama Moja.
1.2. Kadi mbili za Njano (Kadi nyekundu isiyo ya Moja kwa moja) hupunguza alama 3.
1.3. Kadi nyekundu hupunguza alama 4.
1.4. Timu ikipata kadi nyekundu na njano katika mchezo waliokutana hupunguza alama 5.

NB Hata hivyo kama watalingana Kamati ya FIFA wataamua wenyewe yupi awe wa kwanza na yupi wa pili. Fifa hutumia kigezo cha kadi nyingi za njano au kurusha shilingi hewani.

Kwa Haraka haraka Ureno hawana kadi nyekundu wala kadi mbili za njano. Katika mchezo wa kwanza Hispania kupitia kiungo wake Busquets alipewa kadi ya njano ya kwanza. Bila shaka kama Ureno na Hispania watalingana basi Ureno ataongoza kundi.

Ureno wanakwenda kukutana na Iran wakiwa na rekodi ya kutoka hatua ya makundi mara moja katika historia ya kombe la dunia. Rekodi hii ni ya mwaka 2002. Walitoka hatua ya makundi wakiwa wamefunga mabao 6 tu. Walikuwa kundi Moja na Korea Kusini, Marekani na Poland.

Mwaka Huu Marekani hawapo Kombe la dunia, Poland wameshatoka, na hali ya Korea kufuzu ni tete huku Ureno ikisubiri mchezo wa mwisho. Takwimu zinasema Mwaka 2002 Argentina alikuwa Kundi moja ma Nigeria kama ilivyo kwa sasa. Ureno walikuwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Wenyeji Korea ambao ilikuwa ni lazima washinde mchezo huo ili kufikisha alama 7 na kumpiku Marekani. Kibaya zaidi Ureno walipoteza mtanange huo kwa bao Moja pekee.

Je Ronaldo atawavusha leo? Kazi kwake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here