Home Kimataifa RUS 2018: Hary Kane Moto, James Moto.

RUS 2018: Hary Kane Moto, James Moto.

9861
0
SHARE

Colombia 3-0 Poland
James Rodriguez amefunga magoli 6 na kutengeneza mengine manne katika michuano yote ya kombe la dunia. Amezidi kuwa na kiwango murua kabisa. James amecheza kwa kujiamimi mno na kuonesha kwamba yeye ni kiungo wa hadhi ya juu.

Falcao Radamel anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu yake ya taifa. Goli kipa wa zamani wa Colombia El coco alikuwepo uwanjani. El coco ndiye yule golikipa aliyeokoa mpira wa Davies kwa staili ya Scorpion kick (kubetuka kwa nyuma)

Kufikia sasa katika michezo miwili Poland hawajafunga bao lolote licha ya kwamba wanaongozwa na mshambuliaji hatari wa Bayern Munichen Roberto Lewandowski.

England 6-1 Panama.
Hary Kane Hary Kane Hary Kane! Leo ameweka rekodi yake katika kombe la dunia. Hat trick yake ya kwanza huku akiwa mchezaji wa tatu mweny hatrick katika taifa la Uingereza. England tayari wameshakata tiketi ya kwenda hatua ya 16 bora.

Rafiki yangu mmoja ameniambia hawa Panama ni vituko. Bora hata Kenya ya akina wanyama ingeshiriki. Kiwango cha Panama sio kizuri lakini kwao kushiriki kombe la dunia ni historia. Ni tofauti kama tunavyowaza sisi. Hii inajenga motisha kwa taifa lao kwa vizazo vijavyo.

Japan 2-2 Senegal
Senegal wanazidi kuweka rekodi yako katika kombe la dunia ya kutokufungwa mchezo wowote kufikia sasa katika hatua ya makundi. Wamecheza michezo 7 katika historia yao ya kombe la dunia, wakiwa mwashafunga idadi ya mabao 9. Hawajafungwa na timu yoyote ya ulaya.

Kundi hili bado gumu sana.
Senegal alama 4
Japan alama 4
Colombia alama 3
Poland 0

Poland amekwisha kutoka. Mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Senegal na Colombia. Senegal watahitaji Alama 1 tu au tatu lakini Colombia wao wafahitaji ushindi au alama 1 kisha Japan afungwe mchezo wa mwisho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here