Home World Cup RUS2018: Wakimbizi watoa kipigo cha mbwa koko kwa mahasimu wao

RUS2018: Wakimbizi watoa kipigo cha mbwa koko kwa mahasimu wao

13739
0
SHARE

GRANIT Xhaka na Xherdan Shaqiri waliibamiza Serbia mabao mawili kwa moja. Wote walishangilia mabao yao huku wakionesha Ishara za alama za bendera ya nchi yao ya asilia Albania.

Hivi juzi juzi mashabiki wa Uingereza wameonakana wakionesha ishara za heshima za alama za NAZI. Shirika la usalama la England lilikataza mashabiki wake kufanya tukio lolote la kisiasa au kusimama karibu na mnara wa St George ambao zamani ulijulikana kama Stalingrad. Mnara huo ulitajwa kuwa sehemu kubwa ya mauaji hasa hasa wakati wa vita vya pili vya dunia.

Wakati waingereza wanaogopa machafuko ya kisiasa, Xhaka na Shaqiri wao wanakaza roho zao. Wanaamua kuwadhihaki watu waliowafanya wakimbizi.

Baada ya kufunga mabao kila mmoja aliweka viganja vyao vya mikono pamoja huku vidole gumba vikielekea juu kuonesha ishara ya tai wawili ambao ni ishara inayopatikana kwenye bendera ya Albania.

Shaqiri ni mzaliwa wa Kosovo, ambapo zamani lilikuwa jimbo la Serbia kabla ya kuamua kujitawala mwaka 2008. Serbia haijawahi kulitambua jimbo hilo kama taifa linalojitegemea na huru na wamekuwa katika mvutano mkubwa wa kisiasa.

Xhaka wazazi wake ni wazaliwa wa Kosovo na wana asili ya Albania. Wote walivaa Viatu vgenye bendera ya Uswisi na Albania wakienzi mataifa yao halisi.

Kocha wao mkuu bwana Petkovic hakupendezwa kabisa na staili ile ya ushangiliaji ya wachezaji wake.

Tukio kama hili lilitokea mwaka 1941 ambapo vita vya pili vya dunia vilishika Kasi. Wakati ule michuano ya Olympic ilifanyika nchini Ujerumani. Uwanja mzima ulijaa bendera za NAZI ambapo kilikuwa chama cha kifashisti chini dikteta wa kihistoria Mtaasisi Adolf Hitler. Katika Mashindano yale Uingereza walikutana na Ujerumani. Sakata lilianza kwamba kila timu lazima ipite mbele ya Hitler. Ili kumfurahisha Hitler lazima uweke salamu ya heshima. Ikumbukwe mwaka 1934 kuna klabu ilipigwa marufuku baada ya kukataa kutoa salamu hiyo.

Timu ya taifa ya Uingereza ilifanya kitendo ambacho kocha wa Uswisi amekipinga kwa wachezaji wake kukifanya.

Waingerea na kikosi chao wote walipiga saluti mbele ya Hitler. Waziri mkuu wa Uingereza Chamberlain alikerwa sana na kitendo kile. Uwanja ulijaa zaidi ya watu laki moja na kilikuwa kitendo cha fedheha kwa taifa kubwa kama Uingereza kuinama mbele ya Hitler.

Xhaka na Shaqir wameisujudu Albania kocha wao amesema hataki kuona siasa michezoni.

“Hatupaswi kuchanganya mpira na siasa, sio jambo zuri wala halijakaa kimichezo,”

“Ni kweli kwamba walitawalia na hisia. Tunapaswa kujilinda sana na mambo ya nje ya uwanja. Tunapaswa kuwekeza macho yetu kwenye soka hili linalounganisha watu.” Alisema kocha

Shaqiri alizomewa sana kipindi cha kwanza na mashabiki wa Serbia kabla hajawafunga midomo.

“Kwenye mpira kuna mambo mengi, kiukweli nilishikwa na hasira sana kwa sababu mashabiki wao walikuwa wananizomea na wewe mwenyewe umeona kilichotokea,” Alisema Shaqiri.

“Nina furaha kufunga bao sina cha zaidi.”

Qaush Behra ambaye ana asili ya Kosovo alisema amefurahishwa sana na ushindi ule na kudai kuwa alitamani sana alipize kisasi kwa Serbia kwani walisababisha apoteze kazi na ndugu zake walikufa kwenye vita vilivyotokea katika jimbo la Pristina.

Xhaka alisema baba yake alifungwa jela wakati wa utawala wa Slobodan Milosevic kisha alipoachiliwa wote walikimbia taifa hilo.

Zaidi ya maelfu ya wakazai wa Kosovo mnamo mwaka 1998-1999 waliathirika sana na vita wakisaidiwa na na jeshi la Albania kudhibiti jeshi la Serbia. Familia za Behrami, Xhaka na Shaqiri walikimbilia uhamishono nchini Switzerland na kuishi kama wakimbizi.

Haijulikani idadi kamili ya wakimbizi lakini inakadriwa zaidi ya watu 200,000 kutoka Kosovo wanaishi Switzerland, huku Kosovo ikikadiriwa kuwa na watu milioni 1.8

Jamii ya watu wa Kosovo wanaoshi Ujerumani na mataifa mengine wanachangia kiasi cha 175 millioni hela ya Uswisi francs ( Ambayo ni sawa na Yuro miliom 152 , $176 million) kwa ajili ha wakosovo kila mwaka.

Waziri mkuu wa Kosovo Mh Ramush Haradinaj pia alikuwahi kuishi Switzerland, akiwa anafanya kazi kama baunsa na mchezaji wa judo (kung fu au karate) hapo zamani kabla hajarudi Kosovo.

Wakati wa ugombi wa Yugoslavia watu zaidi ya 13,500 walipoteza maisha Kati yao 10,000 walikuwa watu wa Kosovo Albanian.

Shirika la kujihami la NATO Lilipua kambi ya Milosevic na kusambaratisha jeshi lake lote. Miaka 10 baadae Kosovo ilitambulika kama taifa jipya mwaka 2008. Belgrade alikataa katakata kulitambua taifa hilo na amekuwa akisaidia sana Urusi. Xhaka na Shaqiri wapo Urusi ambapo Urusi yenyewe hawalitambui jimbo la Kosovo kama jimbo huru

Belgrade pia alikataa katakata taifa hilo kuruhusiwa kushiriki katika michezo ya kimataifa ya soka.

Kosovo baadae ilitambulika kama mwanachama halisi wa kamati ya mashindano ya Olympic mwaka 2014 kisha baadae UEFA na miaka mwili baadae wakatambuliwa na FIFA

Mwaka huu mwezi mei Serbia aliweka kipingamizi kwa timu ya karate ya Kosovo karate kuingia nchini humu kushiriki mashindano ya Ulaya kule jijini Novi Sad.

“Watu wa Kosovo wote tulikuwa kwenye Tv kufurahia Serbia kupewa kipigo cha mbwa koko,” Alisema mwalimu Daut Maloku, mwemye 46, aliliambia shirika la AFP.

“Uswisi wakishinda na sisi Kosovo tu ashinda,” Alisema Qahil Halili.

“Switzerland ni kikosi chetu cha tatu, Cha kwanza ni Kosovo na cha pili ni Albania,” alisema Halili, mzaliwa wa kijiji cha Zhegra, kijiji alichozaliwa Shaqiri.

Katika mji hamlet mashariki mwa Kosovo unajulikana kama “Switzerland ndogo” ambapo inasema familia 450 wote ni ndugu na ni wenyeji wa Usiwsi.

“Sisi kama wakosovo tunafurahia ushindi wa uswisi kuliko hata Waswisi wenyewe,” Alisema mwandishi wa habari Shkumbin Sekiraqa akanikumbusha ushindi wa nigeria umewafurahisha waargentine kuliko Nigeria wenyewe. Kwa mtazamo wangu sioni kama kuna shida ya kisiasa kiasi cha Waingereza kuandika barua FIFA wakitaka Uswisi waadhibiwe. Kuna jamaa mmoja Muingereza amaeandika barua kwa fifa akitaka wapigwe faini. Faini ya nini watu wameomesha ishara ya mataifa yao asilia? Wao wameonesha bendera ya taifa lao asilia je unamnyima mtu uhuru wa kujivunia asilia yake?

Makala na Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here