Home World Cup RUS2018: Huyu Hazard Huyu! Neymar akasome

RUS2018: Huyu Hazard Huyu! Neymar akasome

12559
4
SHARE

Ubelgiji haina mafanikio makubwa kwenye dunia ya soka. Mafanikio yao makubwa ni mwaka 1920 walipotwaa medali ya dhahabu ya Olympic. Kizazi chao hiki kipya cha akina Witsel, Thibaut na Tielemens ni kizazi kipya kabisa ambacho Javier Martinez hapaswi kusema kikosi changu hakijabalansi.

Baada ya michezo miwili Ubelgiji wananipa sababu ya kubadilisha gia angani. Kuna Kuna kila sababu kuamini kuwa Ubelgiji ina uwezo mkubwa wa kuifunga timu yoyote ile.

Hazard anaonekana kucheza mpira mzuri sana na wenye tija kwa timu. Kuna tofauti kubwa sana unapokuwa na Neymar kwenye timu yako tofauti na Hazard. Sawa Neymar ana mafanikio makubwa timu ya taifa na klabu kuliko Hazard lakini Hazard anacheza kitimu tofauti na mpira wa maji taka wa Neymar.

Takwimu za haraka haraka Neymar amecheza michezo 18 ya kufuzu kombe la dunia pamoja na kombe la dunia kwa mwaka 2018. Amefunga mabao 7, na kuasisti 9.

Hazard amecheza michezo 10 (wa mwisho wa Tunisia). Aemfunga mabao 7 na kuasisti 6. Utagundua aina ya uchezaji wa Hazard na haya anayofanya basi utagundua Hazard amekuwa na msururu mzuri wa ufanisi kwa taifa lake ukilinganisha na Neymar Jr.

Ushindi wa Mabao matano wa Ubelgiji kwa leo ni salamu tosha kwa timu kubwa zinazoyumba yumba kama Argentine, Brazil na zingine. Sawa Ubelgiji amekutana na timu nyepesi lakini hata Argentine Brazil zimekutana na timu nyepesi na zimekwama tu. Kombe la dunia la mwaka huu sio lelemama. Wanaume wamejikaza na wamejiandaa.

Wakati Gabriel Jesus akirukaruka na jezi yake namba 9, Lukaku yeye anaweka historia. Ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza tokea 1986 kufunga mabao mawili katika mchezo mmoja kwenye michezo miwili mfululizo ya kombe la dunia.

Pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ublegiji kufunga magoli manne katika kombe la dunia mojaz na pia amewekea rekodi ya kufunga mabao mengi timu ya taifa katika michuano ya ulaya na kombe la dunia akiwa na mabao saba.

Ubelgiji imejaliwa na wachezaji wenye maarifa makubwa sana hasa hasa Kevin De Bruyne. Bila shaka wamekamilika na wanaweza kutusapraizi.

Uzuri wana timu yenye nidhamu nzuri ya uchezaji. Haina majina makubwa sana ila ina wachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa na ambao wana majukumu ya kutegemewa katika vilabu vyao.

Hawana mpira wa ubishoo. Angalia mtu kama Dembele utagundua kwamba wana timu ya kazi.

Neymar ana kazi kubwa sana na Brazil. Kila mchezaji wa Brazil anaujua mpira haswa. Yaani hawabahatisshi kama Lingard na Welbeck. Yaani ni Mafundi waliokamilika. Shida kila mchezaji anacheza kivyakevyake. Shida hii inaanzia kwa Neymar mwenyewe. Hilo ni tatizo kwa timu kwa ujumla. Neymar anapaswa kubadilika.

Hazard sio mchoyo, hana mambo mengi. Anachohitaji ni timu kupata matokeo. Kila mchezaji wa Chelsea anatamana Hazard aendelee kubakia klabuni hapo. Sina uhakika kama kila mchezaji wa PSG anatamani kuendelea kumuona Neymar klabuni hapo.

Enewei Kila la kheri kwao. By Privaldinho

Comments

comments

4 COMMENTS

  1. Hazard anauwezo mkubwa sana lakini pia sio mchoyo. Kila mchazi anatamani kucheza na Hazard. After row, Hazard anaangalia mafanikio ya tim kwanza baadae yeye.

  2. Comment:Huwez rnganisha MTU aliekua nje ya uwanja takribani miez 3 na m2 alie kwenye fomu..Jr anaingia World Cup angari bado hayuko vzuri ni umuhmu wake tu ulio mlinda so kua makini unapo fananisha..

  3. Comment:Previnho kweli ww ni bonge la mchambuzi maana ukisema alikua majeruhi sio sawa hata Barcelona hayo uliyoyasema Matokeo yake akamuona messi ni mchawi kwake.

  4. Hazard fundi kuliko neymar namtakia wachukue Word cup 2018 hazard goal goal goal neymar hamna kitu yule ubishoo tu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here