Home World Cup RUS2018: Chicharito kwenye mtihani mwingine

RUS2018: Chicharito kwenye mtihani mwingine

9904
0
SHARE

Leo jumamosi, kutakuwa na mchezo wa kundi F Kati ya South Korea, dhidi ya Mexico mchezo huo utapigwa majira ya saa 12 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.mchezo utapigwa Katika dimba la Rostov Arena.

South Korea, mchezo wao wa Kwanza kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Sweden, huku wakitegemea mshambuliaji wao Hyeon- Wao, pia wakitegemea beki wao wa pembeni Kim Wao, akirudi baada ya mchezo wao dhidi ya Sweden, alipata majeruhi.

Kiungo wa South Korea, Jung Woo Young, akielezea mchezo wao dhidi ya Mexico.

“Mexico, wana wachezaji ambao wana kasi na pia wapo vizuri katika mpira wa kupenyeza katika lango la mpinzani”,.

“Angalia mechi yao dhidi ya Ujerumani, pia tunaamini Mexico, watacheza tofauti dhidi ya yetu.na sisi hatuendi kucheza Kama Ujerumani,”.

“huwezi kuzifananisha timu mbili katika karatasi lakini zinatakiwa zipate matokeo uwanjani,”.

“Tunafikiri jinsi ya kumzuia Mexico, asicheze mpira wale wa kushambulia,”.

Mexico, mchezo wao wa Kwanza walishinda dhidi ya Mabingwa watetezi Ujerumani, kwa bao 1-0. Kikosi chetu kimejiandaa vema dhidi ya South Korea.

Kocha wa Mexico, Juan Carlos Osario, akielezea mchezo wao dhidi ya South Korea.

“huu ni muda wa Mexico kuonyesha kuwa timu bora kwa sasa,”.

“kuna utofauti mkubwa kati ya Ujerumani, na timu zengine tunatakiwa kupambana zaidi,”.

Tukumbuke.

Mara ya mwisho hizi timu mbili zilivokutana Mwaka 1998, fainali za kule Ufaransa, Mexico, waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

South Korea, ajashinda michezo saba ya kombe la dunia amepoteza michezo mitatu mfululizo.

Mexico, wamepoteza michezo Miwili Kati ya michezo 18 katika hatua ya makundi ushindi 9, sare 7.

Vikosi vinavoweza kuanza leo.

South Korea. Cho, Y. Lee, H. Jong, Y. Kim, W. Jung, J. Lee, S. Ki, J.Koo, H. Hwang, S. Kim, H. Son.

Mexico. Ochoo, Solcedo, Ayala, Moreno, Gallardo, Herrera, Guadradro, Layun, Vela, Lazano, Jernandez.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here